268-Aayah Na Mafunzo: Tofauti Ya Taathira Ya Shaytwaan Na Ya Malaika Kwa Mwana Aadam

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Tofauti Ya Taathira Ya  Shaytwaan Na Ya Malaika Kwa Mwana Aadam

 www.alhidaaya.com

 

 

الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾

268. Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu, (ubakhili), na Allaah Anakuahidini maghfirah kutoka Kwake na fadhila. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

Mafunzo:

 

‘Abdullaah bin Mas‘uwd  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika shaytwaan humwathiri mwana wa Aadam na Malaika pia humauthiri. Ama kuhusu athari za shaytwaan ni kutisha kwa mambo ya shari na kukadhibisha haki. Ama athari za Malaika ni ahadi ya mwisho mwema na kuamini haki. Yeyote anayeoona haya (athari za Malaika) basi ajue kuwa ni kutoka kwa Allaah na Amhimidi Allaah. Na anayeona ya mwanzo basi aombe kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan.” Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma: “Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu, (ubakhili), na Allaah Anakuahidini maghfirah kutoka Kwake na fadhila.” [Ibn Haatim (3/1090) katika Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share