003-Aayah Na Mafunzo: Mayahudi Kuithamini Aayah Leo Nimekukamilishieni Dini yenu…

Aayah Na Mafunzo

Al-Maaidah

Mayahudi Kuithamini Aayah Leo Nimekukamilishieni Dini yenu…

 

 

 

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣﴾

3. Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah katika kuchinjwa kwake, na aliyenyongwa au aliyepigwa akafa, au aliyeporomoka, au aliyepigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama mwitu, isipokuwa mliyewahi kumchinja kihalali (kabla ya kufa); na waliochinjwa kwa ajili ya ‘ibaadah ya waabudiwa, na kupiga ramli kwa mishale. Hayo kwenu ni ufasiki. Leo wamekata tamaa wale waliokufuru katika Dini yenu; basi msiwaogope, na Niogopeni Mimi. Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. Basi atakayelazimika katika njaa kali bila kuinamia kwenye dhambi (akala vilivyoharamishwa) basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

Mafunzo:

 

Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Myahudi mmoja alimwambia: Ewe Amiri wa Waumini, lau ingeliteremka kwetu sisi Aayah hii Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu.” (5: 3) tungeliifanya ‘Iyd siku hiyo. ‘Umar akasema: Wa-Allaahi, naijua siku gani imeteremka Aayah hii. Imeteremka Siku ya ‘Arafah siku ya Ijumaa. [Al-Bukhaariy].

Share