113-Asbaabun-Nuzuwul: Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan   113-Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako

 

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

113. Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba: (Siku moja) Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) aliichelewesha Swalaah ya ‘Ishaa kisha akatoka kuja kuiswali Masjid akawakuta Maswahaba  (رضي الله عنهم) bado wamemsubiri akasema: “Uhakika wa mambo ulivyo hakuna yoyote katika Watu wa Dini hizi anayemdhukuru Allaah katika wakati huu asiyekuwa nyinyi.” Hapo ikateremka Aayah: Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi…” mpaka mwisho wa Aayah 115. [Hadiyth ya Ibn Mas’uwd ameipokea Al-Imaam Ahmad].

 

Share