128-Asbaabun-Nuzuwul: Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan 128- Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au   

 

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

128. Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba: Alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoinua kichwa chake kutoka rukuu’ ya Swalaah ya Alfajir: “Allaahumma Rabbanaa Lakal-Hamdu fil-Aakhirah. Kisha akasema: “Allaahumma mlaani fulani na fulani.” Ikateremka: Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.”(3: 128) [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo].

Na Anas bin Maalik  (رضي الله عنه)amehadithia kwamba: Siku ya Uhud, jino la Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) lilivunjika na akachomwa mkuki begani mwake. Damu ikawa inamchirizika usoni mwake akawa anaifuta damu huku akisema: “Vipi watu watafaulu ikiwa wamerowanisha uso wa Nabiy wao kwa damu na hali yeye anawalingaia kwa Allaah?” Hapo ikateremka Aayah hii: Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.” (3: 128) [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh].

Share