006-Asbaabun-Nuzuwul: Na Wajaribuni Mayatima (Akili Zao) Mpaka Wakifikia Umri...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

 

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

An-Nisaa  006-Na wajaribuni mayatima (akili zao) mpaka wakifikia umri...

 

وَابْتَلُوا الْيَتَامَىٰ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغُوا النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُوا إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَأْكُلُوهَا إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُوا ۚ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ فَأَشْهِدُوا عَلَيْهِمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٦﴾

6. Na wajaribuni mayatima (akili zao) mpaka wakifikia umri wa kuoa. Na mkihisi kupevuka kwao, basi wapeni mali zao. Wala msiile kwa israfu na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliyekuwa tajiri basi ajizuilie (kuchukua ujira); na aliyekuwa fakiri basi ale kwa kadiri ya kukubalika ki-shariy’ah. Mtapowapa mali zao washuhudizeni. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye kuhisabu.

 

 

Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka ikiwa inabainisha hukmu kuhusu mali ya yatima. Mlezi wa yatima huyo anapokuwa ni fakiri, basi anaweza kula katika mali hiyo kwa wema bila ya israaf. [Amehadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Share