Skip navigation.
Home kabah

Kula Tambuu Inafaa?

 

 

 

SWALI:

Assalam alaykum
Je kula tambuu inafaa kwa sababu kuna watu waliokuwa wanakula mirungi wamiacha lakini sasa wanakula tambuu

 



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Llaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani ndugu yetu kwa swali lako hilo kuhusu vileo. Hakika tunawapatia heko na hongera hao ndugu zetu ambao wameweza kuacha mihadarati mairungi, madawa ya kulevya na pombe na kadhalika. Hii ni ishara kuwa ikiwa mtu anataka kubadilika na kujigeuza katika maovu anaweza kwa tawfiki ya Allah (Subhaanahu wa Ta'ala), kwani yeye Ametuambia: “Hakika Allah habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao” (13: 11).

Tufahamu kuwa Uislamu umewka misingi katika mas-ala ya mihadati na mabo mengine ya haramu na halali. Katika hayo ni kuwa kinacholewesha kwa wingi kidogo pia ni haramu. Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atueleza: “Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo mna madhara makuu na baadhi ya manufaa kwa watu. Lakini madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa” (2: 219). Kwa hiyo, kuharamishwa kwa ulevi ni kuwa madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa. Hii ni kanuni katika Uislamu, ikiwa kitu kina madhara makubwa huwa hakifai kutumiwa na Muislamu.

Hebu tutizame tambuu ina faida gani kwa mwanadamu. Tambuu si lishe yenye kumsaidia mwanadamu kwa chochote huenda ikawa ina nisba ya vitu kidogo sana kwa manufaa yake. Lakini tizama tambuu hiyo ina vitoeo gani, rangi, tumbaku ya majani yaliyokaushwa, chokaa na vyenginezo. Tumbaku mwanzo ni haramu kwani madhara yake ni makubwa zaidi kwa afya ya mwanadamu. Ikiwa sigara ambayo imetolewa baadhi ya kemikali inapotengenezwa ina madhara mengi seuze majani yenyewe. Chokaa pia ina madhara na tambuu yenyewe pia ina madhara kwa mwanadamu anayetumia. Mbali na kuondoa unadhifu kwa kutupa mate ovyo ovyo pindi mtu anapokuwa anakula. Uislamu wenyewe umejengewa na sifa ya unadhifu na usafi.

Hivyo, ni vyema mtu asiwe ni mwenye kula tambuu hata ikiwa bila ya vitoeo vyake.

Na Allah Anajua zaidi