01-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Ameamka Huku Anasinzia Akala Chakula Kisha Akatambua Kuwa Alfajiri Imeshaingia

Ameamka Huku Anasinzia Akala Chakula Kisha Akatambua Kuwa Alfajiri Imeshaingia

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Niliamka asubuhi moja huku bado nusu nimelala (nasinzia) nikaenda jikoni haraka na kula chakula, lakini nilivyoanza kula, nimetazama saa nikaona kuwa ni saa 10: 45 Alfajiri  Na wakati wa Alfajiri  huku Tabuk (Kaskakazini Saudi Arabia) ni 10: 15 Alfajiri. Kwa hiyo nikasimama kula na kuanza kufunga, nikijua kuwa nimekula kama vijiko vitatu au vinne. Je, Sheikh inanipasa nilipe Swawm hii au hainipasi?

 

 

JIBU:

 

Kama hali ni kama ulivyoeleza, basi inakupasa ulipe siku hiyo kwani ulikula baada ya wakati wa Alfajiri kupita.

 

Allaah Atujaalie At-Tawfiyq.  Swalah na Salaam ziwe juu ya Nabiy wetu Muhammad, familia yake, na Maswahaba zake.

 

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. - Fataawaa Ramadhwaan - Mjalada 2, Uk 569, Fatwa Namba 552]
 

 

 

Share