02-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kafara Ngapi Ikiwa Amejimai Zaidi Ya Mara Moja Kwa Siku Moja Ramadhwaan

Kafara Ngapi Ikiwa Amejimai Zaidi Ya Mara Moja Kwa Siku Moja Ramadhwaan

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ikiwa mtu amejimai (kitendo cha ndoa) zaidi ya mara moja katika siku moja ya Ramadhwaan, Je, Anatakiwa alipe kafara mara zile zile sawa na kitendo cha jimai? 

 

 

JIBU:

 

Inavyofahamika katika madhehebu ya Imaam Ahmad ni kwamba ikiwa mtu amejimai zaidi ya mara moja kwa siku moja katika Ramadhwaan basi kafara moja tu inatosheleza. Lakini kama kajimai katika siku mbili za Ramadhwaan (au zaidi ya siku mbili) basi inampasa alipe kafara sawa na siku alizojimai kwa sababu kila siku moja ni tofauti na nyingine (kwa hiyo kila siku moja  ni kafara moja).

 

 

[Imaam Ibn ‘Uthyamiyn - Fataawaa Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa  608, Fatwa Namba 601-Fiqh al-'Ibaadaat]  

 

 

Share