Vitumbua Vidogodogo Vya Yai -2

Vitumbua Vidogodogo Vya Yai -2

 

 

 

Vipimo

 

Mchele          2 mugs

Hamira 1 kijiko cha kulia

Sukari  ¼ robo magi takriban

Tui la nazi zito 2 mugs

Yai 1

Hiliki ½ kijiko cha chai

Mafuta ya kupikia vitumbua

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Roweka mchele masaa mengi uwezavyo.
  2. Chuja maji yamalizike mchele uwe mkavu.
  3. Weka katika blender, kisha tia tui la nazi kidogo kidogo usage mpaka usagike.
  4. Malizia tuni kusagia pamoja na sukari, hamira na vitu vyote vinginevyo.
  5. Mimina katika bakuli funika uumuke.
  6. Weka mafuta kidogo kidogo katika chuma cha vitumbua kisha teka mteko umimine katika kila kishimo.
  7. Vikigeuka rangi upade wa chini, kigeuze kwa kijiti cha mshikaki upike upande wa pili.
  8. Epua uchuje katika chujio kisha katika kitchen tissue. Vikiwa tayari.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share