Swalaah Za Sunnah Muakkadah (Zilizosisitizwa) Na Ghayr Muakkadah (Zisizosisitizwa)

Swalaah Za Sunnah Muakkadah (Zilizosisitizwa) Na Ghayr Muakkadah (Zisizosisitizwa)

 

Fadhila za Swalaah za Sunnah kwa ujumla ni nyingi, mojawapo ni Hadiyth:

 

عَنْ عبادةَ بنِ الصَّامِتِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّهُ سَمِعَ النَبيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْجُدُ للهِ سَجْدَةً إِلاَّ كَتَبَ اللهُ لَهُ بِهَا حَسَنَةً . وَمَحَا عَنْهُ بِهَا سَيِّئَةً ، وَرَفَعَ لَهُ بِهَا دَرَجَةً ، فَاسْتَكْثِرُوا مِنَ السُّجُودِ))

Imepokelewa kutoka ‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) ((Mja yeyote atakayesujudu sijda moja ataandikiwa hasanah (jema) mmoja, na atafutiwa baya moja, na atapandishwa daraja yake, kwa hiyo zidisheni kusujudu)) [Ibn Maajah]  

 

 

Fadhila za kuswali Swalaah za Sunnah Muakkadah (zilizosisitzwa) kabla ya Swalaah au baada ya Swalaah, jumla yake ni rakaa 12 kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

 

(( مَا مِنْ عبْدٍ مُسْلِم يُصَلِّي للَّهِ تَعَالى كُلَّ يَوْمٍ ثِنْتَيْ عشْرةَ رَكْعَةً تَطوعاً غَيْرَ الفرِيضَةِ ، إِلاَّ بَنَى اللَّه لهُ بَيْتاً في الجَنَّةِ ، أَوْ : إِلاَّ بُنِي لَهُ  بيتٌ في الجنَّةِ  )) رواه مسلم  

 ((Hatoswali mja Rakaa 12 zisizo za fardhi kwa siku, ila atajengewa [na Allaah] nyumba Jannah)) [Muslim]

 

Alfajiri:

 

1-Muakkadah: Rakaa 2 kabla ya Swalaah

Suwrah za kusomwa: Suwratul-Kaafiruwn na Suwratul-ikhlaasw

Au Al-Baqarah 2:136 na Aal-‘Imraan 3:64 au Aal-‘Imraan 3:52.

 

Fadhila zake:

 (( ركْعتا الفجْرِ خيْرٌ مِنَ الدُّنيا ومَا فِيها ))   رواه مسلم

((Rakaa mbili (za Sunnah) kabla ya Alfajiri ni kheri kuliko duniya na yaliyomo ndani yake) [Muslim]

 

Bonyeza kiungo upate faida zaidi:

 

Swalah Ya Sunnah Ya Alfajiri Inaswaliwa Vipi Na Wakati Gani? Na Surah Zipi Zisomwe?

 

 

Adhuhuri:

 

2-Muakkadah:  Rakaa 4 kabla ya Swalaah na  rakaa 2 baada ya Swalaah

Ghayr Muakkadah:  Rakaa 2 baada ya Swalaah

 

Alasiri:

 

Hakuna Swalaah za Sunnah.

 

Magharibi:

 

3-Muakkadah: Rakaa 2 baada ya Swalaah unasoma Suwratul-Kaafiruwn na Suwratul-Ikhlaasw.

 

Bonyeza kiungo upate faida zaidi:

 

Surah Gani Zisomwe Swalah Ya Alfajiri Na Magharibi? Inafaa Kusoma Surah Kubwa Na Ndogo?

 

Ghayr Muakkadah: Rakaa 2 baada ya Swalaah.

 

‘Ishaa:

 

4-Muakkadah:  Rakaa 2 baada ya Swalaah

Ghayr Muakkadah: Rakaa 2 kabla ya Swalaah

 

Swalaah Nyenginezo Zilizosisitzwa:

 

5-Swalaah ya Tahajjud:

 

Ni Swalaah bora kabisa baada ya Swalaah za fardhi kwa dalili:

 

(( أَفْضَلُ الصَّلاةِ بَعْدَ الْفَرِيضَةِ صَلاةُ اللَّيْلِ))  رواه مسلم

((Swalah iliyo bora kabisa baada ya Fardh ni Swalah ya usiku))  [Muslim]

 

Bonyeza viungo upate faida zake:

 

Wakati Wa Swalah Ya Tahajjud Na Vipi Kuswali

 

Nini Fadhila Za Swalah Ya Tahajjud?

 

6-Swalaah Ya Dhwuhaa:

 

Ni Swalaah inayoanza kuswaliwa baada ya kuchomoza jua vizuri mpaka karibu na adhuhuri kabla ya kuingia kwake.

Idadi ya Rakaa zake kuanzia 2 hadi 8

Fadhila zake:

عـَن أبي ذَرٍّ رضي الله ُ عنه ، عن النـَبي ِّ صلـَّى الله عليه وسلم قال: ((يـُصـْبـِحُ عـَلى كـُلِّ سـُلامى مـِنْ أحـَدِكـُمْ صـَدَقةُ: فـَكُل تـَسْبـِيحـَةِ صـَدَقةٌ ،وَ كُل تـَحمِيدة صـَدَقةٌ ، وكُلُ تـَهْـليْلةٌ صـَدَقـَةٌ، وكُلُّ تـَكْبِيْرةِ صـَدقةٌ ، وأمرٌ بالمـَعرُوف صـَدقةٌ ، ونـَهىٌ عـَنِ المـُنْكرِ صـَدقةٌ ويـُجْزئ مـِنْ ذلكَ رَكـْعتـَانِ يـَركَعُهُما مـنَ الضـُّحى))  رواه مسلم

Kutoka kwa Abu Dharr (Radhiya Allahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) amesema: ((Kila kiungo katika mwili wenu hupambaukiwa kikihitaji kutolewa sadaka, kwa hiyo kila tasbiyh (kusema ‘SubhaanaAllah’) ni sadaka na kila tahmiyd (kusema ‘AlhamduliLlaah’) ni sadaka na kila tahliyl (kusema ‘La Ilaaha Illa Allah’) ni sadaka  na kila takbiyr (kusema ‘Allahu Akbar’) ni sadaka na kuamrisha mema ni sadaka na kukataza maovu ni sadaka na itamtosheleza (Mtu) kwa Rakaa mbili za Dhuhaa)) [Muslim]

 

Na pia bonyeza kiungo upate faida zaidi:

 

Swalah Ya Dhwuhaa - Rakaa Zake, Fadhila Zake na Wakati Wake

 

 

7- Swalah Ya Witr:

 

 Ni Swalaah inayoswaliwa kuanza baada ya Swalaah ya ‘Ishaa mpaka kabla ya Swalaah ya Alfajiri.

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ : أَوْصَانِي خَلِيلِي صلى الله عليه وسلم بِثَلاثٍ : صِيَامِ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ، وَرَكْعَتَيْ الضُّحَى، وَأَنْ أُوتِرَ قَبْلَ أَنْ أَنَامَ .

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba “Ameniusia rafiki yangu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mambo  matatu; kufunga swawm siku tatu katika kila mwezi, rakaa mbili za dhwuhaa, na niswali Witr kabla ya kulala” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Bonyeza viungo kwa faida ziada:

 

Swalah Ya Witr Inaswaliwa Vipi Na Vipi Kutia Nia?

 

Surah Gani Kusoma Katika Swalah Ya Tahajjud Na Witr?

 

 

 

 

Share

Comments

9

ASSALAM ALEYKUM, NASHKURU KUONA WEBSITE HII, KWANI NATUMAINI ITAWAFUNZA WATU ,HASWA WANAWAKE MAMBO MENGI WASIOYAJUA ,JAZAKALLAHU KHER MAASALAM.

ALLAH AWAPE KILA LA KHEIR. ALHIDAAYA

ASSALM ALEHKUM

NAPENDA KUWASHUKURU KWA KUTUFAHAMISHA KUHUSU DINI YETU YA KISLAM.

JE KUNAFADHILA GANI UKISWALI KATIKA MSIKITI WA MTUME MADINA

ASANTEN SANA

wa 'alaykumus-salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh

Tunashukuru kuwa unafaidika na mafunzo ya Dini yako kupitia Alhidaaya.

Ama kuhusu swali lako, tafadhali tuma kupitia maswali@alhidaaya.com upate kujibiwa katika e-mail yako. Hapa ni mahali pa kuweka maoni yanayohusu makala unayoisoma hapa.

Ndugu Zako
AL HIDAAYA

ASALAAMU ALEYKUM,
NAWAOMBEA KHEYR AL-HIDAYA NA ALLAH SUBHANA TAALA AWAZIDISHIE..AMIN

Assalamu alykum wa rahmatullah wa barakat ..napenda kuwashukuru saana na kuwapongeza ndugu zetu (AL-HIDAAYA.COM)kwa kujitolea kutufunza na kutuelimisha waislaam wote amabao baadhi yetu bado hatujaifahamu vizuri dini yetu ya kiislaam .vile vile napenda kutoa maoni yangu juu yenu (AL-HIDAAYA.COM) kuwa msichoke kwa kazi hii adhimu .Inshallah Allah atakusaidieni kwa kukufanyieni wepesi kufanya kazi hii .Na Allah atawalipeni malipo mema hapa duniani na kesho yaumul qiyama .Aaaamin .

Ahsaante .
wenu mpendwa
YASSER bin HAROUB .

Assalam waleykum warahmatulah wabarakatu.allah awazidishie kila la kheri mzidi kutupa mafundisho yahusuyo dini yetu ya kiislam wallahi nimejifunza mengi nisiyoyajua kupitia alhidaaya allah awatie nguvu mzidi kutuelimisha zaidi.wabillah tawfiq

Assalaamu alaykoum Warahma tul Allah wabartakat, ningependa kuwapongeza sana ndugu zangu popote pale mlipo na nimefurahi sana leo katika mihangaiko yangu ya kuperuzi na kukutana na hii page, Wallahi Allahu yaalam, napenda sana kazi yenu, Allah ndo Atawalipa kwa kheri apa Duniani na kesho Akhera In Shaa Allah, Allahumma amin

Alhamdolellah rabb al3alameen. Namshkuru Allah kwa kunipa waswaa wa moyo kwani nilikuwa na dhiki sana(iliokuwa imesababishwa na kuwa mbali na Allah) lakini baada ya kuingia katika hii website yenu nimenufaika sana na namhimidi Allah kwa kunionyesha njia ya haki. Mungu awafungulie kila milango ya kheri humu duniani na kesho Akhera.