Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi

Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi

 

 

Vipimo 

 

 

Unga vikombe 2 ¼

Siagi 250g

Sukari kukaribia kikombe ½ (au takriban vijiko 10 vya kulia)

Baking powder ½ kijiko cha chai

Ute wa yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Sukari Ya Kunyunyizia na rangi mbali mbali.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Kagawa sukari katika vibakuli utie rangi mbali mbali uweke kando.
  2. Changanya siagi na sukari katika mashine ya kusagia keki upige mpaka ilainike iwe nyororo.
  3. Tia ute wa yai vanilla uhanganye vizuri.
  4. Tia unga na baking powder kidogo kidogo uchanganye upate donge.
  5. Sukuma donge ukate kwa kibati cha shepu ya kopa.
  6. Pakaza siagi katika treya ya kupikia kwenye oveni upange biskuti
  7. Nyunyizia sukari za rangi rangi kisha pika katika oven moto mdogo wa baina 180 – 190 deg F kwa takriban robo saa.
  8. Epua zikiwa tayari.

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share