18-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Du’aa Ya Mwezi Wa Rajab Sha’baan na Ramadhwaan Haikuthibiti

Du’aa Ya Mwezi Wa Rajab Sha’baan na Ramadhwaan Haikuthibiti

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Je, ni Sunnah kusoma du’aa:

اللهم بارك لنا في رجب وشعبان و بلغنا رمضان .

“Ee Allaah Tubarikie katika Rajab na Sha’baan na Tufikishe Ramadhwaan”

 

 

JIBU:

 

Haikuthibiti fadhila za Rajab katika Hadiyth Swahiyh, wala haikuthibiti kufadhilisha mwezi wa Rajab na Jumaadaa Al-Aakhirah ambao ni mwezi wa kabla yake, isipokuwa ni mwezi mtukufu tu! 

 

Wala hakuna Swiyaam iliyowekewa Shariy’ah wala Swalaah wala ‘Umrah wala chochote kile.

 

Mwezi wa Rajab ni kama miezi mingineyo tu. 

 

 

[Liqaa Al-Baab Maftuwh (26/174)]

 

 

Share