08-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Je, I’tikaaf Ya Mwanamke Ni Sawa Na Ya Mwanaume?

Je, I’tikaaf Mwanamke Ni Sawa Na Ya Mwanaume?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

08-Je, I’tikaaf Ya Mwanamke Ni Sawa Na Ya Mwanaume?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

I’tikaaf ya mwanamke ki-shariy’ah ni sawasawa na ya mwanaume lakini tu iambatane na sharti kwamba haitomsababisha ufisadi au fitnah. Pindi itakaposababisha kuwa ni ufisadi au fitnah basi hapo hapaswi kufanya I’tikaaf. Au kama I’tikaaf itamsababisha asiwe na (majukumu na) watoto wake nyumbani mwake au asitimize haki za mumewe basi hapaswi kufanya I’tikaaf.

 

 

[Nuwr ‘Alaa Ad-Darb]

 

 

Share