33-Fatwa: Zakaatul-Fitwr Imewajibika Kwa Mtu Asiyefunga Ramadhaan Kwa Dharua

 Zakaatul-Fitwr Imewajibika Kwa Mtu Asiyefunga Ramadhaan Kwa Dharua?

 www.alhidaaya.com

SWALI:

 

Je, Zakaatul-Fitwr inawajibika kwa mtu aliyekuwa hakufunga Ramadhaan kwa sababu alikuwa katika safari au mgonjwa?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Rai za wengi miongoni mwa ‘Ulamaa pamoja na Maimaam wanne na wengineo ni kwamba Zakaatul-Fitwr inawajibika kwa Muislamu hata kama hakufunga Ramadhwaan. Hakuna mwingine aliyekhitilafiana isipokuwa Sa'iyd bin Muswayyab na Hasan Al-Baswriy ambao wamesema kuwa Zakaatul-Fitwr inawajibika kwa wale waliofunga pekee. Lakini rai iliyo sahihi ni rai ya wengi wao kwa kutokana na dalili zifuatazo:

 

1-Maana kwa ujumla ya Hadiyth ambayo asili yake ni kuwa Zakaatul-Fitwr ni fardhi.

Imesimuliwa kwamba Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kwa swaa’ ya tende, au swaa’ ya shayiri (ngano) kwa kila mtu, mtumwa au aliye huru, mwanamume au mwanamke, mdogo au mkubwa na ameamrisha kwamba ilipwe kabla ya watu kwenda kuswali" [Al-Bukhaariy (1503) na Muslim (9840]

Neno la 'mdogo' inajumuisha watoto wadogo ambao hawawezi kufunga.

 

 

2- Sadaka na Zakaah zinapoamrishwa kawaida ni kwa ajili ya kuwasaidia watu masikini na wanaohitaji na inakusudiwa kupatikana upeo fulani wa hifadhi ya jamii. Iliyo dhahiri kwa kusudio hili ni Zakaatul-Fitwr ambayo imeamrishwa kwa wadogo na wakubwa, aliye huru na mtumwa, mwanamume na mwanamke na mtoaji sheria hakubainisha thamani ya chini kabisa (Niswaab) au muda wa mwaka kuwa ni fardhi.

 

Hivyo kwa vile ni fardhi kwa wale ambao hawakufunga Ramadhwaan, ikiwa ni kutokana na sababu au bila ya sababu, inaonyesha sababu ya kuwekwa kwa sheria ya Zakaah.  

 

 

 3- Kuhusu mabishano ya wale walionukuu kama ni dalili ya maneno ya Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kama ni kumtakasa mwenye kufunga kutokana na maneno ya upuuzi na machafu na kuwalisha masikini" [Abuu Daawuwd (1609)]

 

Wamesema: Maneno 'kama ni kumtwaharisha mtu aliyefunga' ina maana kwamba Zakaatul-Fitwr ni fardhi kwa wale waliofunga. Al-Haafidhw Ibn Hajar amejibu hivyo katika Al-Fat-h (3/369) ambako kasema:

 

"Jibu langu ni kwamba kutaja ‘kutakaswa’ kunamaanisha hali ya kawaida (kwa watu wengi ilivyo) kama vile inavyohitajika kwa wale ambao hawakutenda dhambi, mfano Wachaji Allaah au ambaye amekuwa Muislamu dakika kabla ya jua kuzama." [mwisho wa kunukuu].

 

Inayokusudiwa ni kwamba katika hali nyingi Zakaatul-Fitwr imefaridhishwa katika shariy'ah kwa sababu ni twahara ya aliyefunga, lakini kupatikana twahara si sharti inayoifanya kuwa ni fardhi. Mfano kama Zakaah ya mali ambayo pia imefaridhishwa kwa ajili ya kutwaharisha nafsi:

 

((Chukua swadaqa katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rahmah. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Allaah ni Mwenye kusikia Mjuzi)) [At-Tawbah: 103].

 

Juu ya kwamba Zakaah ni fardhi katika hali ya mali inayomilikiwa na mtoto mdogo ambaye hahitaji kutwaharisha nafsi, kwa sababu hakuna vitendo vibaya vinavyoandikwa kwa ajili yake. 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share