079-Asbaabun-Nuzuwl: An-Naazi'aat Aayah 42-46: يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا

 

 

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

079-An-Naaziaat 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾

42. Wanakuuliza (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa lini kufika kwake?

 

 

فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾

43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.

 

 

 

 
 

Ibn Jariyr (30/49) amesema: Amenihadithia Ya’quwb bin Ibraahiym amesema: Ametuhadithia Sufyaan bin ‘Uyaynah kutoka kwa Az-Zuhriy kutoka kwa ‘Urwah kutoka kwa ‘Aaishah amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliendelea kuulizia kuhusu Saa hadi Allaah Alipoteremsha:
 

فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾

43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.

 

 

Hadiyth imepokewa na Al-Hakam katika Al-Mustadrak (1/5) na Abuu Nu’aym katika Al-Hilyah (7/314) na akasema Al-Hakam Hadiyth hii haikuwepo katika Asw-Swahihayn nayo ni mahfuwdhw Swahiyh juu ya sharti zao wawili. Na akasema ni Swahiyh kwa sharti zao na hawakuipokea kwa sababu Ibn ‘Uyaynah aliifanyia Irsaal kwa mwingine na Al-Khatwiyb (11/321).

 

Na Al-Haafidhw ameitaja Hadiyth hii ibn Abiy Haatim katika kitabu chake Al-‘Ilal, na akasema nimemsikia Aba Zur’ah  na akataja Hadiyth ya Az-Zuhriy kutoka kwa ‘Urwah kutoka kwa ‘Aaishah amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliendelea kuuliza kuhusu Qiyaamah hadi ilipoteremka kwake:

 فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾

43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.

 

 

 

Na amesema Ibn Jariyr (رحمه الله) :Ametuhadithia Abuu Kurayb, ametuhadithia Waki’y kutoka kwa Ismaa’iyl kutoka kwa Twaariq bin Shihaab amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaendelea kutaja mambo ya Qiyaamah hadi ilipoteremka:

 يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾

42. Wanakuuliza (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa lini kufika kwake?

 

Hadi kauli yake:

   مَن يَخْشَاهَا ﴿٤٥﴾

wa yule anayeikhofu.

 

 

Adh-Dhahabiy Al-Haythamiy (رحمه الله)  amesema: Ameipokea Al-Bazaar na watu wake ni Swahiyh (7/133) kutoka katika Al-Majma’ na akasema Al-Hafidhw Ibn Kathiyr (رحمه الله) katika tafsiyr yake (2/273) baada ya kutaja kwake sanad na isnad hii ni nzuri na yenye nguvu.

 

 

Aayah Husika Za Asbaabun-Nuzwul:

 

 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾

42. Wanakuuliza (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa lini kufika kwake?

 

 

فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾

43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.

 

 

إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا ﴿٤٤﴾

44. Kwa Rabb wako ndio kuishia (ujuzi) wake.

 

 

إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا ﴿٤٥﴾

45. Hakika wewe ni muonyaji wa yule anayeikhofu.

 

كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا ﴿٤٦﴾

46. Siku watakapoiona, watakuwa kama kwamba hawakubaki (duniani) isipokuwa jioni moja au mchana wake.

 

 

Share