073-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muzzammil: يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ

 

 

 

Sababu Za Kuteremshwa

(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Suwrah Al-Muzzammil

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

073-Al-Muzzammil

 

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾

1. Ee uliyejifunika.

 

 

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ مُحَمَّدٍ،  يَعْنِي الْمَرْوَزِيَّ حَدَّثَنَا وَكِيعٌ، عَنْ مِسْعَرٍ، عَنْ سِمَاكٍ الْحَنَفِيِّ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ أَوَّلُ الْمُزَّمِّلِ كَانُوا يَقُومُونَ نَحْوًا مِنْ قِيَامِهِمْ فِي شَهْرِ رَمَضَانَ حَتَّى نَزَلَ آخِرُهَا وَكَانَ بَيْنَ أَوَّلِهَا وَآخِرِهَا سَنَةٌ.  صحيح  الألباني

Ahmad bin Muhammad ametuhadithia (yaani Al-Marwaziyy), Waki’y ametuhadithia kutoka kwa Mis’ar kutoka kwa Simaak Al-Hanafiyy kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Pindi ilipoteremka mwanzo wa Muzzammil walikuwa wanasimama kama visimamo vya vya Ramadhwaan hadi ilipoteremka ya mwisho wake na muda wa kuteremka Aayah ya kwanza hadi ya mwisho ilikuwa ni mwaka mzima. [Sunan Abiy Daawuwd – Kitaab At-Tatwawwa’ – Mlango Wa Kufuta Qiyaam Al-Layl Na Wepesi wake- Ameisahihisha Al-Albaaniy - Wapokezi wa Hadiyth ni watu Swahiyh isipokuwa Ahmad bin Muhammad Al-Marwaziyy Abal Hassan bin Shabawayhi naye ni thiqqah (mwenye kuaminika), Imepokewa na Ibn Jariyr (29/124-125) na wapokezi wake ni Sahihi. Na imepokewa na Ibn Abiy Haatim kama katika Tafsiyr Ibn Kathiyr (4/436) na wapokezi wake ni sahihi].

 

 

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾

1. Ee uliyejifunika.

 

قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا﴿٢﴾

2. Simama (kuswali) usiku kucha isipokuwa kidogo tu.

 

نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا﴿٣﴾

3. Nusu yake, au ipunguze kidogo.

 

أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا﴿٤﴾

4. Au izidishe, na soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu upasao, kuitamka vizuri na kutaamali.

 

إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا﴿٥﴾

5. Hakika Sisi Tutakuteremshia juu yako kauli nzito.

 

إِنَّ نَاشِئَةَ اللَّيْلِ هِيَ أَشَدُّ وَطْئًا وَأَقْوَمُ قِيلًا﴿٦﴾

6. Hakika kuamka usiku (kuswali) ni uthibiti zaidi wa kuathiri moyo na kuifahamu na unyofu zaidi wa maneno kutua.

 

إِنَّ لَكَ فِي النَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا﴿٧﴾

7. Hakika una mchana mrefu kwa shughuli nyingi.

 

وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا﴿٨﴾

8. Na dhukuru Jina la Rabb wako, na jitolee Kwake kwa kujitolea kikamilifu.

 

رَّبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلًا﴿٩﴾

9. Rabb wa Mashariki na Magharibi, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Basi mfanye kuwa ni Mdhamini wako.

 

وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا﴿١٠﴾

10. Na subiri juu ya yale wayasemayo, na wahame, mhamo mzuri.

 

Aayah Ya Mwisho Suwrah hii:

 

إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَاللَّـهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ ۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ ۙ وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ ۚ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٢٠﴾

20. Hakika Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Anajua kwamba unasimama (kuswali) karibu na thuluthi mbili za usiku au nusu yake, au thuluthi yake; na kundi miongoni mwa wale walio pamoja nawe. Na Allaah Anakadiria usiku na mchana. Anajua kwamba hamuwezi kuukadiria wakati wake na kusimama kuswali, basi Amepokea tawbah yenu. Basi someni kile kilicho chepesi katika Qur-aan. (Allaah) Anajua kwamba watakuweko miongoni mwenu wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wanatafuta fadhila za Allaah, na wengineo wanapigana katika njia ya Allaah. Basi someni kile kilicho chepesi humo. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mkopesheni Allaah karadhi nzuri. Na chochote kile cha khayr mnachokadimisha kwa ajili ya nafsi zenu, mtakikuta kwa Allaah. Ni bora, na ujira mkubwa zaidi. Na mwombeni Allaah maghfirah, hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

Share