Swalaah Zote Zinanipita Kwa Ajili Ya Kazi Ni Sawa Kuzikidhi?

 

 

SWALI:

Linaambatana na swali la muulizaji kuhusu kufanya kazi ya kuchinja nguruwe.

 Swali langu la pili ni hili kulingana na mida ya kuanza kazi hapa ninalazimika kutoka usiku wa alfajiri kabla swalati subuhi haijingia na kwenda kazini bila kusali subuhi na huko kazini hakuna nafasi ya kusalia na nirudia nyumbani mida ya jioni baada ya salati li-ishai.

  Sasa ninapo fika usiku nalazimia kuzisali zote sala tano kwa pamoja swali langu ni hili hapa jee ninapatiya ao kuna njia ingine naweza kuifata?

    Hayo ndio maswali yangu ma bayo ninataka majibu insha allah.nawatakia kila la kheri na fanaka.

 

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake, Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka siku ya Mwisho.

Shukran kwa swali lako zuri kuhusu nguzo muhimu sana miongoni mwa nguzo za Uislamu. Swalah ndiyo amali ya kwanza itakayotazamwa Siku ya Kiyama. Na Allah (Subhaanahu wa Ta‘alaa) Ameiwekea wakati maalum kwa nguzo hiyo kuweza kutekelezwa pale Aliposema: “Kwani hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu” (4: 103).

Katika sheria mambo ambayo yanaweza kumfanya mtu akidhi Swalah ni matatu ya msingi, nayo ni; kulala, kusahau, na kutenzwa nguvu.

Hivyo inabidi utenge wakati wa kuweza kutekeleza Swalah yako na katika hali hiyo uliyoko sasa ni vigumu kuweza kutekeleza hilo. Inabidi uache kazi hiyo na utafute nyingine, kwani ukiacha kwa ajili ya Allah, Allah (Subhaanahu wa Ta‘alaa) Atakufungulia njia. Allah (Subhaanahu wa Ta‘alaa) Anasema: “Na anayemcha Mwenyezi Mungu Humtengezea njia ya kutokea. Na Humruzuku kwa jiha asiyotazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Yeye Humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu Anatimiza amri Yake. Mwenyezi Mungu Kajaalia kila kitu na kipimo chake” (65: 2 - 3).

Na Allah Anajua zaidi.

 

 

 

 

 

Share