Al-Lajnah Ad-Daa'imah: Maana Ya Salafiyyah Na Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah

Maana Ya Salafiyyah Na Nini Hukmu Ya Kujinasibisha Nayo

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini maana ya Salafiyyah na nini hukmu ya kujinasibisha nayo?

 

 

JIBU:

 

Salafiyyah inatokana na ‘Salaf’ na Salaf ni Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na walioongoka katika watu wa karne tatu za kwanza ambao Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewashuhudia kwa khayr katika kauli yake:

 

“Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia...“   [Imaam Ahmad katika Musnad yake na Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na Salafiyyuwn ni wingi wa Salafiy, (nayo) inatokana na (neno) Salaf na imeshatangulia maana yake.

Nao ni wale ambao wamefuata Manhaj ya Salaf katika kufuata Kitabu na Sunnah na kufanyia da’wah (kuilingania) na kufanyia kazi. Na wakawa kwa hiyo ni Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah.”

 

 

[Fataawaa Al-lajnah Ad-Daaimah (2/243)]

 

 

Share