Kuelekea Wapi Kuswali Ikiwa Hujui Qiblah Kiko Wapi?


SWALI: 

 Ukiwa umehamia mahali ugenini na hujui kibla unaelekea wapi? NI jinsi gani unaweza kujua kibla kilipo kwa kuangalia jua linapochomoza au linapozama???

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ni muhimu kwa Muislamu anaposafiri sehemu ya ugenini angalau ajue jiografia fupi ya sehemu kama hiyo ili asipate shida katika ibadah zake za Swalah anapofika huko. Al-Ka‘bah ndiyo tunayoelekea wakati wa Swalah na Alhamdullillahi kwa sasa ipo miswala ambayo ina dira (‘compass’) pamoja na kijitabu kidogo kinacho kufahamisha namba ya kuelekeza ukiwa katika miji tofauti ulimwenguni. Hii ni njia moja rahisi ya kukutoa katika usumbufu aina yoyote.

Ikiwa huna mswala kama huo basi ni muhimu ujue jiografia japokuwa kidogo. Ikiwa upo Afrika Mashariki, kawaida Qiblah ni kaskazini, hivyo mkono wako wa kuume ukielekea kunapochomoza jua na mkono wa kushoto kunapotua jua basi uso wako utakuwa umeelekea Makkah. Kukusaidia zaidi ni mpaka tujue uko wapi.

 Na Allaah Anajua zaidi

 

Share