18-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Atakayetamka Baada Ya Wudhu ... Atafunguliwa Milango Minane Ya Jannah Aingie Autakao

 Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

 www.alhidaaya.com

 

18-Atakayetamka Baada Ya Wudhu “Ash-hadu An Laa Ilaaha Illa Allaah...

Atafunguliwa Milango Minane Ya Jannah Aingie Autakao

 

عَنْ عُمَرَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم : ((مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ، فَيُسْبِغُ اَلْوُضُوءَ، ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ)) أَخْرَجَهُ مُسْلِم

 

Kutoka kwa ‘Umar (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna yeyote miongoni mwenu anayetawadha vizuri, kisha akasema: “Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, wa ash-hadu anna Muhammad ‘Abduhuu wa Rasuwluhu” (Nashuhudia kuwa hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Peke Yake, hana mshirika, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake) ila atafunguliwa milango minane ya Jannah aingie wowote aupendao kati ya hiyo.” [Imetolewa na Muslim na At-Tirmidhiy]

 

 

Share