06-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Hajj: Mlango Wa Kukosa Hijjah Na Kuzuilika

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْحَجِّ

Kitabu Cha Hajj

 

 

بَابُ اَلْفَوَاتِ وَالْإِحْصَارِ

06-Mlango Wa Kukosa Hijjah Na Kuzuilika

 

 

 

645.

عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ:{قَدْ أُحْصِرَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏فَحَلَقَ‏ وَجَامَعَ نِسَاءَهُ، وَنَحَرَ هَدْيَهُ، حَتَّى اِعْتَمَرَ عَامًا قَابِلًا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alizuiliwa.[1] Kwa hivyo akanyoa kichwa chake, akajamiiana na wake zake, na akachinja wanyama wake. Kisha akafanya ‘Umrah mwaka uliofuata.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

646.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {دَخَلَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏عَلَى ضُبَاعَةَ بِنْتِ اَلزُّبَيْرِ بْنِ عَبْدِ اَلْمُطَّلِبِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي أُرِيدُ اَلْحَجَّ، وَأَنَا شَاكِيَةٌ، فَقَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم "حُجِّي وَاشْتَرِطِي: أَنَّ مَحَلِّي‏ حَيْثُ حَبَسْتَنِي"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliingia kwa Dhwubaa’ah[2] bint Az-Zubayr bin ‘Abdil-Mutwalib (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) na akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nimedhamiria kuhiji lakini ninaumwa.” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Hiji, lakini omba na uweke sharti kuwa: Mahala nitakapovulia Ihraam ndipo Wewe (Allaah) Utakuwa Umenizuia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

647.

وَعَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ اَلْحَجَّاجِ بْنِ عَمْرٍو اَلْأَنْصَارِيِّ‏ رضى الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{مَنْ كُسِرَ، أَوْ عُرِجَ، فَقَدَ حَلَّ وَعَلَيْهِ اَلْحَجُّ مِنْ قَابِلٍ قَالَ عِكْرِمَةُ.‏ فَسَأَلْتُ اِبْنَ عَبَّاسٍ وَأَبَا هُرَيْرَةَ عَنْ ذَلِكَ؟ فَقَالَا: صَدَقَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa ‘Ikrimah[3] amesema kuwa Al-Hajjaaj bin ‘Amr Al-Answaariyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuvunjika mguu au kulemaa, lazima atoke katika hali ya Ihraam na lazima atekeleze Hijjah mwaka unaofuata.” ‘Ikrimah amesema: “Nilimuuliza Ibn ‘Abbaas na Abuu Hurayrah juu ya hilo nao walisema: “Amesema kweli.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na At-Tirmidhiy aliipa daraja la Hassan]

 

[1] Ni mambo gani yanayoweza kuhesabika kuwa kikwazo au kipingamizi katika kufanya Hijjah? Wanazuoni wengi zaidi wana maoni kwamba, chochote kinachoingilia kati Hijjah ya Haaji (mwenye kuhiji) ni kikwazo, iwe ni adui, ugonjwa, vita au kushindwa kusafiri. Wengine wanasema kuwa Ihswaar (kipingamizi) husababishwa na adui tu ambaye kafiri. Kuna kutofautiana miongoni mwa Wanazuoni kuhusu kafara itolewayo na mahujaji wanaopingamizwa kama hao. Wengi wanasema Haaji aliye namna hiyo sharti achinje mnyama wa kafara mahala pale pale anapovulia Ihraam yake, kama mahala hapo pako ndani au nje ya eneo la kuchinja wanyama wa kafara.

[2] Dhwubaa’ah bint Az-Zubayr bin ‘Abdil-Mutwalib alikuwa akiitwa Umm Hakiym Dhwubaa’ah bint Az-Zubayr bin ‘Abdil-Mutwalib bin Haashim bin ‘Abdil-Manaaf, binti wa mjomba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Aliolewa na Al-Miqdaad bin Al-Aswad aliyemzalia ‘Abdullaah na Karimah. Alikufa wakati wa Ukhalifa wa ‘Aliy

[3] ‘Ikrimah muachwa huru wa ‘Abdullaah bin ‘Abbaas asili yake ni mberiberi (watu wa Morocco) ni Mwanachuoni wa Tafsiyr ya Qur-aan. Alifariki mwaka wa 107 A.H.

 

 

Share