06-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Watoto Na Vijana Kutekeleza Hajj Inahesabika Ni Hajj Ya Fardhi?

 

Watoto Na Vijana Kutekeleza   Hajj  Inahesabika Ni Hajj Ya Fardhi?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Nilifanya Hajj nilipokuwa na umri wa miaka kumi, kisha nilifanya tena nikiwa na umri wa miaka kumi na tatu, je inatosheleza kuwa nimetimiza fardhi ya Hajj?

 

 

JIBU:

 

Hajj hizo kama zilivyotajwa zinatosheleza kuwa ni Hajj za fardhi ikiwa zimefanywa baada ya kubaleghe aidha kwa kutokwa na manii ndotoni au kwa kuona nywele kuota sehemu za siri.  Hii ni kwa sababu mwanamume na mwanamke hutambulika kuwa amebaleghe kutokana na matukio hayo mawili. Vile vile kufikia umri wa miaka kumi na tano na kuanza nidhamu ya hedhi kwa mwanamke.

 

 Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 23, Fatwa Namba 10938 - Imejumuisha:

 

Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz ibn 'Abdillaah  ibn Baaz

 

Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfy

 

Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah Ibn Ghudayyaan]

 

 

Share