01-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Wudhuu Kuharibika Wakati Wa Twawaaf Je Arudie Twawaaf?

 

Wudhuu Kuharibika Wakati Wa Twawaaf Je Arudie Twawaaf?

 

 Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nilipokuwa nikifanya twawaaf katika Ka'bah na nilipofika  twawaaf ya tano nilihisi kama nimetokwa na pumzi. Iblisi akanitia wasiwasi lakini nikapuuza kwa sababu sikuwa na hakika na sikusikia harufu. Nikajikinga naye kwa Allaah na nikaweka imani yangu kwa Allaah nikaendelea kufanya twawaaf. Kisha nilipomaliza nikaswali Rakaa mbili. Je twawaaf yangu itakuwa ni sahihi?

 

 

JIBU:

 

 

Hukmu ya asasi ni kuwa kuwa utakuwa umebakia katika hali ya twahara, kwani kutia shaka tu kama umetokwa na pumzi hakumtoi mtu katika twahara mpaka uwe na uhakika. Hivyo twawaaf na Swalaah yako ni sahihi na salama In Shaa Allaah.

 

 

[Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 244, Swali Namba 4 la Fatwa Namba 11935 -   Imejumuisha:

 

Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdul-’Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz

 

Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy

 

Mjumbe: Shaykh ‘Abdullaah bin Ghudayyaan

 

Mjumbe: Shaykh ‘Abdullaah bin Qu’uwd]

 

 

Share