01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Masharti Yake Na Yaliokatazwa

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

 

بَابُ شُرُوطِهِ وَمَا نُهِيَ عَنْهُ مِنْهُ

01-Mlango Masharti Yake Na Yaliokatazwa

 

 

 

 

648.

عَنْ رِفَاعَةَ بْنِ رَافِعٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ سُئِلَ: أَيُّ اَلْكَسْبِ أَطْيَبُ ؟ قَالَ: {عَمَلُ اَلرَّجُلِ بِيَدِهِ، وَكُلُّ بَيْعٍ مَبْرُورٍ}  رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa Rifaa’ah bin Raafi’ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliulizwa: Kazi gani bora zaidi?[1] Akasema: “Ni kazi ya mtu kwa mkono wake, na kila biashara halali.” [Imetolewa na Al-Bazzaar na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

649.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ يَقُولُ عَامَ اَلْفَتْحِ، وَهُوَ بِمَكَّةَ: {إِنَّ اَللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ اَلْخَمْرِ، وَالْمَيْتَةِ، وَالْخِنْزِيرِ، وَالْأَصْنَامِ.  فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ ! أَرَأَيْتَ شُحُومَ اَلْمَيْتَةِ، فَإِنَّهُ تُطْلَى بِهَا اَلسُّفُنُ، وَتُدْهَنُ بِهَا اَلْجُلُودُ، وَيَسْتَصْبِحُ بِهَا اَلنَّاسُ ؟ فَقَالَ: " لَا هُوَ حَرَامٌ "، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عِنْدَ ذَلِكَ: " قَاتَلَ اَللَّهُ اَلْيَهُودَ، إِنَّ اَللَّهَ لَمَّا حَرَّمَ عَلَيْهِمْ شُحُومَهَا جَمَلُوهُ، ثُمَّ بَاعُوهُ، فَأَكَلُوا ثَمَنَهُ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

 Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa alimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema mwaka wa Fat-hi (Ukombozi wa Makkah) akiwa Makkah: “Hakika Allaah Ameharamisha kuuza (au kununua) pombe, mfu, nguruwe na masanamu.” Akaulizwa Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje shahamu ya mfu, kwani majahazi hupakiwa nayo ngozi, hupakwa kwayo na watu wanajiangazia kwayo (wanatia kwenye taa zao). Akasema: “Laa hiyo ni haramu.” Kisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Allaah Awalaani mayahudi. Kwa hakika Allaah Alipowaharamishia shahamu ya mfu, wao waliiyeyusha wakawa wanaiuza; wakala thamani yake.”[2] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

650.

وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ يَقُولُ: {إِذَا اِخْتَلَفَ اَلْمُتَبَايِعَانِ لَيْسَ بَيْنَهُمَا بَيِّنَةٌ، فَالْقَوْلُ مَا يَقُولُ رَبُّ اَلسِّلْعَةِ أَوْ يَتَتَارَكَانِ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ 

Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Wawili wenye kuuziana watakapokhitilafiana na hakuna baina yao ubainifu, basi kauli itakayosikilizwa ni ya mwenye bidhaa, au wote wawili waache (biashara hiyo).” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

651.

وَعَنْ أَبِي مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ ثَمَنِ اَلْكَلْبِ، وَمَهْرِ الْبَغِيِّ، وَحُلْوَانِ اَلْكَاهِنِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Abuu Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza thamani ya mbwa,[3] mahari ya kahaba[4] na bahashishi ya kahini[5] (mpiga ramli).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

652.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّهُ كَانَ  يَسِيرُ عَلَى جَمَلٍ لَهُ أَعْيَا. فَأَرَادَ أَنْ يُسَيِّبَهُ. قَالَ: فَلَحِقَنِي اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَدَعَا لِي، وَضَرَبَهُ، فَسَارَ سَيْراً لَمْ يَسِرْ مِثْلَهُ، قَالَ: " بِعْنِيهِ بِوُقِيَّةٍ " قُلْتُ: لَا. ثُمَّ قَالَ: " بِعْنِيهِ " فَبِعْتُهُ بِوُقِيَّةٍ، وَاشْتَرَطْتُ حُمْلَانَهُ إِلَى أَهْلِي، فَلَمَّا بَلَغْتُ أَتَيْتُهُ بِالْجَمَلِ، فَنَقَدَنِي ثَمَنَهُ، ثُمَّ رَجَعْتُ فَأَرْسَلَ فِي أَثَرِي. فَقَالَ: " أَتُرَانِي مَاكَسْتُكَ لِآخُذَ جَمَلَكَ ؟ خُذْ جَمَلَكَ وَدَرَاهِمَكَ. فَهُوَ لَكْ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ، وَهَذَا اَلسِّيَاقُ لِمُسْلِمٍ 

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Alikuwa juu ya ngamia wake aliyechoka, akataka amuache aende anapotaka. Akasema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaniombea na akampiga (yule ngamia), akaenda mwendo ambao hajawahi kuenda mfano wake. Kisha akasema: Niuzie kwa wakia moja.[6] Nikamuambia: Hapana. Halafu akaniambia: Niuzie. Nikamuuzia kwa wakia moja. Nikashurutisha kunibeba kwake hadi kwa watu wangu (Madiynah). Nilipofika nilimpelekea ngamia. Akalipa thamani yake. Kisha nikarejea. Akatuma mtu nyuma yangu akasema: Wadhani kuwa nimekutaradhilia unipunguzie thamani ili nichukue ngamia wako?[7] Chukua ngamia wako na dirham zako ni milki yako.” [Al-Bukhaariy, Muslim na haya ni maneno ya Muslim]

 

 

 

653.

وَعَنْهُ قَالَ: {أَعْتَقَ رَجُلٌ مِنَّا عَبْداً لَهُ عَنْ دُبُرٍ لَمْ يَكُنْ لَهُ مَالٌ غَيْرُهُ. فَدَعَا بِهِ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَبَاعَهُ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Mtu miongoni mwenu alitangaza kumuacha huru mtumwa wake baada ya kifo chake, alikuwa hana mali isipokuwa mtumwa huyo. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuita na akamuuza[8] (na thamani yake akampa mwenyewe).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

654.

وَعَنْ مَيْمُونَةَ زَوْجِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَرَضِيَ عَنْهَا {أَنَّ فَأْرَةً وَقَعَتْ فِي سَمْنٍ، فَمَاتَتْ فِيهِ، فَسُئِلَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْهَا. فَقَالَ: " أَلْقُوهَا وَمَا حَوْلَهَا، وَكُلُوهُ "}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

وَزَادَ أَحْمَدُ. وَالنَّسَائِيُّ: {فِي سَمْنٍ جَامِدٍ}

Kutoka kwa Maymuwnah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) mke wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Panya aliingia katika samli akafa humo. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaulizwa kuhusu panya yule, akasema: Mtupeni na kilicho kando yake na mle (samli hiyo).” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

Ahmad na An-Nasaaiy wameongeza: “katika samli iliyoganda”

 

 

 

655.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {إِذَا وَقَعَتْ اَلْفَأْرَةُ فِي اَلسَّمْنِ، فَإِنْ كَانَ جَامِداً فَأَلْقُوهَا وَمَا حَوْلَهَا، وَإِنْ كَانَ مَايِعًا فَلَا تَقْرَبُوهُ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَقَدْ حَكَمَ عَلَيْهِ اَلْبُخَارِيُّ وَأَبُو حَاتِمٍ بِالْوَهْمِ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Panya atakapoingia katika samli, ikiwa imeganda basi mtupeni na kilichomo kando yake, na ikiwa ni maji maji msiikaribie.” [Imetolewa na Ahmad, na Abuu Daawuwd, Al-Bukhaariy na Abuu Haatim wamesema ina shaka]

 

 

 

656.

وَعَنْ أَبِي اَلزُّبَيْرِ قَالَ: سَأَلْتُ جَابِرًا عَنْ ثَمَنِ اَلسِّنَّوْرِ وَالْكَلْبِ ؟ فَقَالَ: {زَجَرَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ ذَلِكَ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ  .

وَالنَّسَائِيُّ وَزَادَ: {إِلَّا كَلْبَ صَيْدٍ}

Kutoka kwa Abuu Az-Zubayr[9] amesema kuwa Nilimuuliza Jaabir kuhusu thamani ya paka na mbwa,[10] akasema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikataza jambo hilo.” [Imetolewa na Muslim]

 

Na An-Nasaaiy akazidisha: “Isipokuwa mbwa wa kuwinda.”

 

 

 

657.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {جَاءَتْنِي بَرِيرَةُ، فَقَالَتْ: كَاتَبْتُ أَهْلِي عَلَى تِسْعٍ أُوَاقٍ، فِي كُلِّ عَامٍ أُوقِيَّةٌ، فَأَعِينِينِي. فَقُلْتُ: إِنْ أَحَبَّ أَهْلُكِ أَنْ أَعُدَّهَا لَهُمْ وَيَكُونَ وَلَاؤُكِ لِي فَعَلْتُ، فَذَهَبَتْ بَرِيرَةُ إِلَى أَهْلِهَا. فَقَالَتْ لَهُمْ، فَأَبَوْا عَلَيْهَا، فَجَاءَتْ مِنْ عِنْدِهِمْ، وَرَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ جَالِسٌ. فَقَالَتْ: إِنِّي قَدْ عَرَضْتُ ذَلِكَ عَلَيْهِمْ فَأَبَوْا إِلَّا أَنْ يَكُونَ اَلْوَلَاءُ لَهُمْ، فَسَمِعَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَأَخْبَرَتْ عَائِشَةُ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ . فَقَالَ: خُذِيهَا وَاشْتَرِطِي لَهُمُ اَلْوَلَاءَ، فَإِنَّمَا اَلْوَلَاءُ لِمَنْ أَعْتَقَ فَفَعَلَتْ عَائِشَةُ، ثُمَّ قَامَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فِي اَلنَّاسِ خَطِيباً، فَحَمِدَ اَللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ. ثُمَّ قَالَ: " أَمَّا بَعْدُ، مَا بَالُ رِجَالٍ يَشْتَرِطُونَ شُرُوطاً لَيْسَتْ فِي كِتَابِ اَللَّهِ  مَا كَانَ مِنْ شَرْطٍ لَيْسَ فِي كِتَابِ اَللَّهِ فَهُوَ بَاطِلٌ، وَإِنْ كَانَ مِائَةَ شَرْطٍ، قَضَاءُ اَللَّهِ أَحَقُّ، وَشَرْطُ اَللَّهِ أَوْثَقُ، وَإِنَّمَا اَلْوَلَاءُ لِمَنْ أَعْتَقَ "} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ  .

وَعِنْدَ مُسْلِمٍ فَقَالَ:{اِشْتَرِيهَا وَأَعْتِقِيهَا وَاشْتَرِطِي لَهُمُ اَلْوَلَاءَ} 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Bariyrah[11] (mjakazi) alinijia akasema: Nimeandikiana[12] (kuniacha huru) na mabwana zangu kwa wakia tisa; kila mwaka wakia moja; basi nisaidie. Nikamuambia: Mabwana zako wakipenda niwahesabie (hizo) na walaa[13] wako uwe kwangu nitafanya. Bariyrah akawaendea mabwana wake akawaeleza, wakamkatalia. Akaja kutoka kwako na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameketi. Akasema: nimewaambia jambo hilo wakakataa[14] isipokuwa walaa uwe kwao. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasikia. ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) akasema nikamueleza Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Akamuambia ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا): Mchukue na uwashurutishe walaa, kwani walaa ni wa mwenye kuacha huru.[15] ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) akafanya hivyo kisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasimama katika watu Akamhimidi Allaah na Akamsifu kisha akasema: Ammaa ba’d: wana nini watu wanashurutisha masharti yasiyokuwemo katika Kitabu cha Allaah! Sharti isiyokuwemo katika Kitabu cha Allaah ni batili, hata kama ni masharti mia. Hukumu ya Allaah ina nguvu na mno, na walaa ni wa mwenye kuacha huru.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

Na katika Riwaayah ya Muslim amesema: “Mnunue umuache huru na uwashururutishie walaa.”

 

 

 

658.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَهَى عُمَرُ عَنْ بَيْعِ أُمَّهَاتِ اَلْأَوْلَادِ فَقَالَ: لَا تُبَاعُ، وَلَا تُوهَبُ، وَلَا تُورَثُ، لِيَسْتَمْتِعْ بِهَا مَا بَدَا لَهُ، فَإِذَا مَاتَ فَهِيَ حُرَّةٌ}  رَوَاهُ مَالِكٌ، وَالْبَيْهَقِيُّ، وَقَالَ: رَفَعَهُ بَعْضُ اَلرُّوَاةِ، فَوَهِمَ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “’Umar amekataza kuuza mama wa watoto,[16] akasema: hawauzwi wala hawatolewi hiba, wala hawarithiwi, atastarehe naye anavyotaka, atakapokufa (bwana) mwanamke huyo ni huru.” [Imetolewa na Maalik na Al-Bayhaqiyy]

 

 

 

659.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {كُنَّا نَبِيعُ سَرَارِيَنَا، أُمَّهَاتِ اَلْأَوْلَادِ، وَالنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ حَيٌّ، لَا نَرَى بِذَلِكَ بَأْسًا} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikuwa tukiuza vijakazi wetu mama wa watoto, na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) yuko hai, haoni ubaya kwa hilo.” [Imetolewa na An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ad-Daaraqutwniy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

660.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {نَهَى اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ بَيْعِ فَضْلِ اَلْمَاءِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَزَادَ فِي رِوَايَةٍ: {وَعَنْ بَيْعِ ضِرَابِ اَلْجَمَلِ}

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuza ziada ya maji.”[17] [Imetolewa na Muslim]

 

Na katika Riwaayah nyingine akaongeza: “Na kuuza mapigo ya ngamia.”[18]

 

 

 

661.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ عَسْبِ اَلْفَحْلِ}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza mapigo ya ngamia.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

662.

وَعَنْهُ، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ بَيْعِ حَبَلِ اَلْحَبَلَةِ، وَكَانَ بَيْعاً يَتَبَايَعُهُ أَهْلُ الْجَاهِلِيَّةِ: كَانَ اَلرَّجُلُ يَبْتَاعُ اَلْجَزُورَ إِلَى أَنْ تُنْتَجَ اَلنَّاقَةُ، ثُمَّ تُنْتَجُ اَلَّتِي فِي بَطْنِهَا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema tena kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuza mimba ya wenye mimba (Habalil-habalah),[19] na (hiyo) ilikuwa ni biashara wanayouziana watu wa jahiliya. Mtu alikuwa ananunua ngamia mpaka azaliwe ngamia koo kisha kizaliwe kilichomo tumboni mwake.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

663.

 وَعَنْهُ، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ بَيْعِ اَلْوَلَاءِ، وَعَنْ هِبَتِهِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema tena kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuza walaa[20] na kuutoa hiba.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

664.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ بَيْعِ اَلْحَصَاةِ، وَعَنْ بَيْعِ اَلْغَرَرِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza biashara ya kurusha kijiwe na biashara ya udanganyifu.”[21] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

665.

وَعَنْهُ: أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {مَنِ اِشْتَرَى طَعَاماً فَلَا يَبِعْهُ حَتَّى يَكْتَالَهُ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kununua chakula, asikiuze mpaka akipime.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

666.

وَعَنْهُ قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ بَيْعَتَيْنِ فِي بَيْعَةٍ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ  

وَلِأَبِي دَاوُدَ: {مَنْ بَاعَ بَيْعَتَيْنِ فِي بَيْعَةٍ فَلَهُ أَوَكَسُهُمَا، أَوْ اَلرِّبَا}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza mauzo mawili katika uzo moja.”[22] [Imetolewa na Ahmad na An-Nasaaiy na akaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan]

 

Na katika Riwaayah ya Abuu Daawuwd inasema: “Yeyote mwenye kuuza mauzo mawili katika uzo moja, basi ima atapata kilicho kichache kati ya viwili au riba.”[23]

 

 

 

667.

وَعَنْ عَمْرِوِ بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا يَحِلُّ سَلَفٌ وَبَيْعٌ وَلَا شَرْطَانِ فِي بَيْعٍ، وَلَا رِبْحُ مَا لَمْ يُضْمَنْ، وَلَا بَيْعُ مَا لَيْسَ عِنْدَكَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ، وَالْحَاكِمُ 

وَأَخْرَجَهُ فِي " عُلُومِ اَلْحَدِيثِ " مِنْ رِوَايَةِ أَبِي حَنِيفَةَ، عَنْ عَمْرٍو اَلْمَذْكُورِ بِلَفْظِ: " نَهَى عَنْ بَيْعٍ وَشَرْطٍ " وَمِنْ هَذَا اَلْوَجْهِ أَخْرَجَهُ اَلطَّبَرَانِيُّ فِي " اَلْأَوْسَطِ " وَهُوَ غَرِيبٌ 

Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb amepokea kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Si halali kujumuisha mkopo na mauzo,[24] wala masharti mawili katika uzo moja,[25] wala faida katika mali asiyodhamini, wala kuuza kitu usichokimiliki.”[26] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha At-Tirmidhiy, Ibn Khuzaymah na Al-Haakim]

 

Al-Haakim ameitaja katika ‘’Uluwmul-Hadiyth’ kutoka kwa Abuu Haniyfah naye kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kwa tamko: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza biashara (iliyochanganywa) iliyokokotezwa kwa sharti.” Atw-Twabaraaniyy ameitaja katika mnyororo wa wapokezi hawa katika Al-Awsatw, na ni Hadiyth ghariyb (iliyotajwa na mpokezi mmoja tu).

 

 

 

668.

وَعَنْهُ قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ بَيْعِ اَلْعُرْبَانِ}  رَوَاهُ مَالِكٌ، قَالَ: بَلَغَنِي عَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، بِهِ

Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kutoka kwa baba yake na babu yake amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza biashara ya ‘Urbaan.”[27] [Imetolewa na Maalik ambaye amesema: Imenifikia (akitaja mnyororo wa wapokezi wake) kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb]

 

 

 

669.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {اِبْتَعْتُ زَيْتاً فِي اَلسُّوقِ، فَلَمَّا اِسْتَوْجَبْتُهُ لَقِيَنِي رَجُلٌ فَأَعْطَانِي بِهِ رِبْحاً حَسَناً، فَأَرَدْتُ أَنْ أَضْرِبَ عَلَى يَدِ اَلرَّجُلِ، فَأَخَذَ رَجُلٌ مِنْ خَلْفِي بِذِرَاعِي، فَالْتَفَتُّ، فَإِذَا هُوَ زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ، فَقَالَ: لَا تَبِعْهُ حَيْثُ اِبْتَعْتَهُ حَتَّى تَحُوزَهُ إِلَى رَحْلِكَ; فَإِنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى أَنْ تُبَاعَ اَلسِّلَعُ حَيْثُ تُبْتَاعُ، حَتَّى يَحُوزَهَا اَلتُّجَّارُ إِلَى رِحَالِهِمْ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nilinunua mafuta sokoni, nilipokabidhiwa alikuja mtu (hapo hapo) akanipa faida nzuri, nami nikataka kumuuzia, mara mtu mmoja akanishika kwa nyuma yangu, nilipogeuka alikuwa Zayd bin Thaabit, akasema: Usiuze mahala uliponunua hadi uchukue mahali pako, kwani hakika Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amakataza bidhaa kuuzwa mahali inaponunuliwa mpaka wafanya biashara wazipeleke maeneo yao (wazikabidhi).”[28] [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd, matni ya Hadiyth ni yake. Na wakaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]

 

 

 

670.

وَعَنْهُ قَالَ: {قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي أَبِيعُ بِالْبَقِيعِ، فَأَبِيعُ بِالدَّنَانِيرِ وَآخُذُ اَلدَّرَاهِمَ، وَأَبِيعُ بِالدَّرَاهِمِ وَآخُذُ اَلدَّنَانِيرَ، آخُذُ هَذَا مِنْ هَذِهِ وَأُعْطِي هَذَهِ مِنْ هَذِا ؟ فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: لَا بَأْسَ أَنْ تَأْخُذَهَا بِسِعْرِ يَوْمِهَا مَا لَمْ تَتَفَرَّقَا وَبَيْنَكُمَا شَيْءٌ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Mimi ninauza ngamia Baqiy’ nikiuza kwa dinari na nikichukua dirham, na nikiuza kwa dirham na nikichukua dinari, nachukua dirhamu badala ya dinari.  Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Si vibaya kuchukua kwa bei ya siku ile[29] madamu hamujaachana na baina yenu kitu kipo.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

671.

وَعَنْهُ قَالَ: {نَهَى صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنِ النَّجْشِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kupandishana bei katika biashara.”[30] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

672.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ اَلْمُحَاقَلَةِ، وَالْمُزَابَنَةِ، وَالْمُخَابَرَةِ، وَعَنْ اَلثُّنْيَا، إِلَّا أَنْ تُعْلَمَ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا اِبْنَ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza Muhaaqalah,[31] Muzaabanah,[32] Mukhaabarah[33] na Ath-Thun-yaa ila itakapojulikana.”[34] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ahmad) isipokuwa Ibn Maajah, na akaisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

 

673.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنِ اَلْمُحَاقَلَةِ، وَالْمُخَاضَرَةِ، وَالْمُلَامَسَةِ، وَالْمُنَابَذَةِ، وَالْمُزَابَنَةِ}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza Muhaaqalah, Mukhaadhwarah,[35] Mulaamasah,[36] Munaabadhah[37] na Muzaabanah.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

674.

 وَعَنْ طَاوُسٍ، عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا تَلَقَّوْا اَلرُّكْبَانَ، وَلَا يَبِيعُ حَاضِرٌ لِبَادٍ ". قُلْتُ لِابْنِ عَبَّاسٍ: مَا قَوْلُهُ: " وَلَا يَبِيعُ حَاضِرٌ لِبَادٍ ؟ " قَالَ: لَا يَكُونُ لَهُ سِمْسَارًا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Twaawus[38] kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msiwapokee wasafiri, wala mkazi wa mjini asiuze kwa niaba ya mtu wa mashambani.[39] Nikamuambia ‘Abdullaah bin ‘Abbaas: Nini makusudio ya kauli yake “Wala mkazi wa mjini asiuze kwa niaba ya mtu wa mashambani?” Akasema: Asiwe dalali wake.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

675.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا تَلَقَّوا اَلْجَلَبَ، فَمَنْ تُلُقِّيَ فَاشْتُرِيَ مِنْهُ، فَإِذَا أَتَى سَيِّدُهُ اَلسُّوقَ فَهُوَ بِالْخِيَارِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msiwapokee wasafiri, atakayepokezwa bidhaa ikanunuliwa kwake, basi atakapokuja mwenyewe sokoni ana khiyari (ya kutoivunja biashara).” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

676.

وَعَنْهُ قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَنْ يَبِيعَ حَاضِرٌ لِبَادٍ، وَلَا تَنَاجَشُوا، وَلَا يَبِيعُ اَلرَّجُلُ عَلَى بَيْعِ أَخِيهِ، وَلَا يَخْطُبُ عَلَى خِطْبَةِ أَخِيهِ، وَلَا تُسْأَلُ اَلْمَرْأَةُ طَلَاقَ أُخْتِهَا لِتَكْفَأَ مَا فِي إِنَائِهَا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلِمُسْلِمٍ: {لَا يَسُمِ اَلْمُسْلِمُ عَلَى سَوْمِ اَلْمُسْلِمِ}  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza mkazi wa mjini kumuuzia kwa niaba mtu wa kijijini, wala msipandishiane bei,[40] wala mtu asiuze juu ya biashara ya nduguye, wala asipose juu ya posa ya nduguye (Muislam), wala mwanamke asiombe dada yake kupewa talaka ili afaidike kwa kuachwa kwake.”[41] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Wala Muislam asinunue juu ya biashara ya Muislam (mwenzake).”[42]

 

 

 

677.

وَعَنْ أَبِي أَيُّوبَ اَلْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ يَقُولُ: {مَنْ فَرَّقَ بَيْنَ وَالِدَةٍ وَوَلَدِهَا، فَرَّقَ اَللَّهُ بَيْنَهُ وَبَيْنَ أَحِبَّتِهِ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَالْحَاكِمُ، وَلَكِنْ فِي إِسْنَادِهِ مَقَالٌ وَلَهُ شَاهِدٌ 

Kutoka kwa Abuu Ayyuwb Al-Answaariy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Mwenye kufarikisha baina ya mama na mtoto wake, Allaah Atafarikisha baina yake na vipenzi vyake Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha At-Tirmidhiy na Al-Haakim

 

 

 

678.

وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {أَمَرَنِي رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَنْ أَبِيعَ غُلَامَيْنِ أَخَوَيْنِ، فَبِعْتُهُمَا، فَفَرَّقْتُ بَيْنَهُمَا، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَقَالَ: أَدْرِكْهُمَا، فَارْتَجِعْهُمَا، وَلَا تَبِعْهُمَا إِلَّا جَمِيعًا} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ، وَقَدْ صَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ، وَالطَّبَرَانِيُّ، وَابْنُ اَلْقَطَّانِ 

Kutoka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniamrisha kuwauza vijana wawili ndugu nikawauza kwa kuwatenga. Kisha nikamuelezea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) jambo hilo. Akaniambia: watafute uwarudishe,[43] wala usiwauze isipokuwa pamoja.” [Imetolewa na Ahmad. Wapokezi wake ni madhubuti. Na wakaisahihisha Ibn Khuzaymah, Ibn Al-Jaaruwd, Ibn Hibbaan, Al-Haakim, Atw-Twabaraani na Ibn Al-Qatwaan]

 

 

 

679.

وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {غَلَا اَلسِّعْرُ بِالْمَدِينَةِ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَقَالَ اَلنَّاسُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ ! غَلَا اَلسِّعْرُ، فَسَعِّرْ لَنَا، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ إِنَّ اَللَّهَ هُوَ اَلْمُسَعِّرُ، اَلْقَابِضُ، اَلْبَاسِطُ، الرَّازِقُ، وَإِنِّي لَأَرْجُو أَنْ أَلْقَى اَللَّهَ تَعَالَى، وَلَيْسَ أَحَدٌ مِنْكُمْ يَطْلُبُنِي بِمَظْلِمَةٍ فِي دَمٍ وَلَا مَالٍ "}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Bei zilipanda Madiynah katika zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) watu wakamuambia: Ee Rasuli wa Allaah! Bei zimepanda, tupange bei. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Kwa hakika Allaah Ndiye Mwenye kuwafikia (Mpanga bei), Mwenye kudhikisha, Mwenye Kukunjua, Mwenye Kuruzuku,[44] mimi nataraji kukutana na Allaah na hali hakuna miongoni mwenu mwenye kunidai kwa kudhulumiwa damu wala mali.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

680.

وَعَنْ مَعْمَرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {لَا يَحْتَكِرُ إِلَّا خَاطِئٌ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Ma’mar bin ‘Abdillaah[45] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amepokea kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuwa amesema: “Halimbikizi ila mkosaji.”[46] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

681.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {لَا تَصُرُّوا اَلْإِبِلَ وَالْغَنَمَ، فَمَنِ اِبْتَاعَهَا بَعْدُ فَإِنَّهُ بِخَيْرِ اَلنَّظَرَيْنِ بَعْدَ أَنْ يَحْلُبَهَا، إِنْ شَاءَ أَمْسَكَهَا، وَإِنْ شَاءَ رَدَّهَا وَصَاعًا مِنْ تَمْرٍ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَلِمُسْلِمٍ: {فَهُوَ بِالْخِيَارِ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ}

وَفِي رِوَايَةٍ: لَهُ، عَلَّقَهَا  اَلْبُخَارِيُّ: {رَدَّ مَعَهَا صَاعاً مِنْ طَعَامٍ، لَا سَمْرَاءَ}

 قَالَ اَلْبُخَارِيُّ: وَالتَّمْرُ أَكْثَرُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msivimbishe chuchu za ngamia na mbuzi (kuonesha yamejaa), na mwenye kumnunua baada ya hapo basi ana khiyari kuchagua moja kati ya mambo mawili, baada ya kumkama; akitaka atabaki nae na akitaka atamrudisha pamoja na pishi ya tende.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “...naye yuko katika khiari kwa muda wa siku tatu.[47] (Ambapo ataamua kuyaweka au hapana).”[48]

Na katika Riwaayah yake nyingine ambayo Bukhaariy ameifanya ni Mu’allaq imesema: “…na atarudisha pamoja na pishi ya chakula isiyokuwa kawahia.”

 

Bukhaariy amesema katika Riwaayah: “Iliyotaja tende ndio iliyopokewa na wapokezi wengi.”

 

 

 

682.

وَعَنِ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ:{مَنِ اِشْتَرَى شَاةً مَحَفَّلَةً، فَرَدَّهَا، فَلْيَرُدَّ مَعَهَا صَاعًا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ  .

وَزَادَ اَلْإِسْمَاعِيلِيُّ:{مِنْ تَمْرٍ}

Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mwenye kununua mnyama aliyevimbishwa chuchu na akamrudisha, basi atakapomrudisha amrudishe pamoja na pishi.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

Na Al-Ismaa’iliyy ameongezea: “…ya tende.”

 

 

 

683.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ مَرَّ عَلَى صُبْرَةِ طَعَامٍ، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فِيهَا، فَنَالَتْ أَصَابِعُهُ بَلَلًا ، فَقَالَ: " مَا هَذَا يَا صَاحِبَ اَلطَّعَامِ ؟ " قَالَ: أَصَابَتْهُ اَلسَّمَاءُ يَا رَسُولَ اَللَّهِ. فَقَالَ: أَفَلَا جَعَلْتَهُ فَوْقَ اَلطَّعَامِ; كَيْ يَرَاهُ اَلنَّاسُ ؟ مَنْ غَشَّ فَلَيْسَ مِنِّي} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipita katika lundo la chakula (nafaka), akaingiza mkono wake ndani, vidole vyake vikagusa unyevu. Akasema: Ee mwenye chakula, ni nini hii? Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Kimepatwa na manyunyu, akamuambia: Si ungekiweka juu ya chakula ili watu wakione! Mwenye kughushi si katika mimi.”[49] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

684.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ بُرَيْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مَنْ حَبَسَ اَلْعِنَبَ أَيَّامَ اَلْقِطَافِ، حَتَّى يَبِيعَهُ مِمَّنْ يَتَّخِذُهُ خَمْراً، فَقَدَ تَقَحَّمَ اَلنَّارَ عَلَى بَصِيرَةٍ}   رَوَاهُ اَلطَّبَرَانِيُّ فِي " اَلْأَوْسَطِ " بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah amepokea kutoka kwa baba yake kuwa amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuhifadhi zabibu msimu wa kuchuma (zabibu) ili amuuzie mtengeneza pombe, kwa hakika atakuwa amejiingiza motoni kwa ujuzi.”[50] [Imetolewa na Atw-Twabaraaniyy katika kitabu chake cha ‘Al-Awsatw’ kwa Isnaad Hasan]

 

 

 

685.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {اَلْخَرَاجُ بِالضَّمَانِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَضَعَّفَهُ اَلْبُخَارِيُّ، وَأَبُو دَاوُدَ وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ، وَابْنُ اَلْقَطَّانِ 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kodi ni kwa dhamana.”[51] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na wameidhoofisha Al-Bukhaariy na Abuu Daawuwd, na wakaisahihisha At-Tirmidhiy, Ibn Khuzaymah, Ibn Al-Jaaruwd, Ibn Hibbaan, Al-Haakim na Ibn Al-Qatwaan]

 

 

 

686.

وَعَنْ عُرْوَةَ الْبَارِقِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَعْطَاهُ دِينَارًا يَشْتَرِي بِهِ أُضْحِيَّةً، أَوْ شَاةً، فَاشْتَرَى شَاتَيْنِ، فَبَاعَ إِحْدَاهُمَا بِدِينَارٍ، فَأَتَاهُ بِشَاةٍ وَدِينَارٍ، فَدَعَا لَهُ بِالْبَرَكَةِ فِي بَيْعِهِ، فَكَانَ لَوْ اِشْتَرَى تُرَابًا لَرَبِحَ فِيهِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ

وَقَدْ أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ ضِمْنَ حَدِيثٍ، وَلَمْ يَسُقْ لَفْظَهُ 

 وَأَوْرَدَ اَلتِّرْمِذِيُّ لَهُ شَاهِداً: مِنْ حَدِيثِ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ

Kutoka kwa ‘Urwah Al-Baariqiyy[52] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa dinari (moja) ili anunulie Udhwhiyyah[53] au mbuzi. Akanunua mbuzi wawili kwa dinari hiyo, mbuzi mmoja akamuuza kwa dinari moja, akaenda kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiwa na mbuzi na dinari. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akambariki katika biashara yake (‘Urwah)[54] akawa lau angenunua mchanga basi angepata faida.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy]

 

Bukhaariy ameileza katika jumla ya Hadiyth nyingine wala hakuitaja tamshi lake.

 

At-Tirmidhiy ametaja ushahidi wake kutoka katika Hadiyth ya Hakiym bin Hizaam.

 

 

 

687.

وَعَنِ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ شِرَاءِ مَا فِي بُطُونِ اَلْأَنْعَامِ حَتَّى تَضَعَ، وَعَنْ بَيْعِ مَا فِي ضُرُوعِهَا، وَعَنْ شِرَاءِ اَلْعَبْدِ وَهُوَ آبِقٌ، وَعَنْ شِرَاءِ اَلْمَغَانِمِ حَتَّى تُقْسَمَ، وَعَنْ شِرَاءِ اَلصَّدَقَاتِ حَتَّى تُقْبَضَ، وَعَنْ ضَرْبَةِ اَلْغَائِصِ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ، وَالْبَزَّارُ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kununua vilivyomo matumboni mwa wanyama mpaka wazae, na amekataza kuuza vilivyomo katika chuchu za wanyama,[55] na kununua mtumwa aliyetoroka, na kununua ghanima mpaka zigawanywe, na kununua Swadaqah mpaka zikadhibiwe, na amekataza kubahatisha mpiga mbizi.”[56] [Imetolewa na Ibn Maajah, Al-Bazzaar na Ad-Daaraqutwniyy kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

688.

وَعَنِ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا تَشْتَرُوا اَلسَّمَكَ فِي اَلْمَاءِ; فَإِنَّهُ غَرَرٌ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَشَارَ إِلَى أَنَّ اَلصَّوَابَ وَقْفُهُ 

Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msinunue samaki akiwemo majini, kwani ni udanganyifu.” [Imetolewa na Ahmad na ameashiria kuwa Hadiyth hii ni Mawquwf (yaani ni maneno ya Swahaba, yaani Ibn Mas-‘uwd)]

 

 

 

689.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَنْ تُبَاعَ ثَمَرَةٌ حَتَّى تُطْعَمَ، وَلَا يُبَاعَ صُوفٌ عَلَى ظَهْرٍ، وَلَا لَبَنٌ فِي ضَرْعٍ}  رَوَاهُ اَلطَّبَرَانِيُّ فِي " اَلْأَوْسَطِ " وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ 

وَأَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ فِي " اَلْمَرَاسِيلِ " لِعِكْرِمَةَ، وَهُوَ اَلرَّاجِحُ.

وَأَخْرَجَهُ أَيْضاً مَوْقُوفاً عَلَى اِبْنِ عَبَّاسٍ بِإِسْنَادٍ قَوِيٍّ، وَرَجَّحَهُ اَلْبَيْهَقِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuza matunda mpaka yaive, wala manyoya kuuzwa juu ya mgongo, wala maziwa katika chuchu.”[57] [Imetolewa na Atw-Twabaraaniyy katika kitabu chake Al-Awsatw na Ad-Daaraqutwniy]

 

Na Abuu Daawuwd katika Al-Maraasiyl kutoka kwa Ikrimah nayo ni yenye nguvu.

 

Vile vile amepokea ikiwa Mawquwf Ibn ‘Abbaas ikiwa na sanadi yenye nguvu na akaipa nguvu Al-Bayhaqiyy.

 

 

 

690.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ بَيْعِ اَلْمَضَامِينِ، وَالْمَلَاقِيحِ} رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ، وَفِي إِسْنَادِهِ ضَعْفٌ

 Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuza mimba katika matumbo ya ngamia,[58] na manii katika migongo ya ngamia.”[59] [Imetolewa na Al-Bazzaar na katika Isnaad yake kuna udhaifu]

 

 

 

691.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مَنْ أَقَالَ مُسْلِماً بَيْعَتَهُ، أَقَالَهُ اَللَّهُ عَثْرَتَهُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kukubali kurudishiwa kile alichomuuzia Muislamu,[60] Allaah atamsamehe dhambi zake.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]

 

[1] Ni kazi gani au chumo gani lililo bora zaidi? Wanazuoni wametofautiana katika hili. Imaam An-Nawawiy amesema: Sawa ni kuwa chumo bora na inayokuwa kwa kazi ya mkono, japokuwa kilimo ni chumo bora kwa kukusanya kazi ya mkono na kutawakali na ndani yake kuna manufaa ya jumla ya wana Aadam, wanyama na ndege. Haafidh bin Hajar amesema: Zaidi ya hivyo ni yanayo chumwa kutokana na mali za makafiri kwenye jihadi, na hilo chumo la Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na hilo ni chumo tukufu zaidi la machumo yote, kwa kuwa ndani yake kuna kuinua neno la Allaah.” Imesemwa Hii inaingia katika chumo la mkono.

[2] Ina maana ya kufanya biashara katika pombe, wanyama wafu, najisi ya maiti na nguruwe, sanamu ni haramu. Hadiyth hii imeweka wazi kuwa faida inayotokana na kitu kilicho haramu ni haramu vile vile, kubadilika kwa namna yake hakuihalalishi kama vile Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alivyohukumu kuhusu faida inayotokana na mafuta.

[3] Kulingana na maoni ya Wanazuoni takriban wote ni kuwa biashara ya mbwa ni haramu.

[4] Mapato yanayotokana na kahaba ni haramu kulingana na maoni ya Wanazuoni wote.

[5] Hul-waan al-kaahin:  Wanazuoni wamekubaliana uharamu wa kumpa kahini, na kahini ni ambaye anadai elimu ya ghaibu na kuwaeleza watu yatakayotokea ni haramu. Hali kadhaalika kuimba na kucheza kwa malipo ya kikahini ni haramu.

[6] Wakia mmoja ni sawa na Dirhaam arubaini.

[7] Yaani labda unadhani kuwa nimenunua ngamia wako kwa thamani ndogo.

[8] Hii ina maana ya kumuuza mtumwa Mudabbar ni jambo lililoruhusiwa. Mtumwa Mudabbar, mwanamme au mwanamke ni yule anayeambiwa na anayemmiliki: “Utakuwa huru baada ya kufa kwangu.”

[9] Jina lake ni Muhammad bin Muslim Tadrus Al-Asadi Al-Makki, muach ahuru wa Hakiym bin Hizaam. Alikuwa ni Taabi’ thiqah aliyekubaliwa na Wanazuoni wa Hadiyth.

[10] Kuuza na kununua paka ni jambo lisiloruhusiwa kishariy’ah. Hivyo hivyo hakuna tofauti kati ya mbwa wa kawaida kuhusu biashara yake kuwa haramu. Hata hivyo mtazamo unakuwa tofauti kuhusu mbwa wa kuwinda, ambapo baadhi ya Wanazuoni wanajuzisha.

[11] Ni mjakazi aliyeachwa huru na ‘Aaishah. Ni Swahaba aliishi hadi katika utawala wa Yaziyd. Aliolewa na Mughiyth, mtumwa katika familia ya Abuu Ahmad bin Jahsh. Alipoachwa huru Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa uchaguzi na akachagua kumuacha mume wake ambae alikuwa mtumwa bado na hivyo akawa ameachika.

[12] Kitaabah au Mukaatabah una maana ya mkataba ulioandikwa wa kumuacha huru mtumwa wa kike au wa kiume kwa mkabala wa malipo. Malipo haya yanaweza kupendekezwa kufanyika katika moja ya pande mbili. Kwa mfano mwenye kumiliki mtumwa akadai malipo mkabala na kumuacha huru mtumwa wake na mtumwa akaaridhi malipo mkabala na uhuru wake.

[13] Walaa: mtumwa aliyeachwa huru. Anapokufa, atarithiwa na yule aliyemuacha huru.

[14] Baada ya kifo cha mtumwa Mukattab (mwanamme au mwanamke) mali aliyoacha huitwa Walaa. Ikitokea mtu akalipa hela ya mkataba na kumuacha huru Mukattab (mtumwa mwanamme au mwanamke) katika hali ya kifo cha mtumwa, yule atakayelipa fedha basi atarithi; lakini ikiwa hela ya mkataba ililipwa na mtumwa mwenyewe mali yake inakwenda kwa jamaa zake.

[15] Ina maana kumuacha huru Mukattab (mtumwa aliyeandika mkataba) kwa gharama fulani inaruhusiwa.

[16] Makusudio ya Ummul-Walad (Mama mtoto) ni mjakazi anaeingiliwa na bwana wake kwa ujakazi na akapata mtoto kwa bwana wake huyo. Mtoto huyo awe ni mume au mke. Ummul-walad (Mama mtoto) atakuwa huru baada ya kufariki bwana wake, wala hastahiki kuuzwa wala kutolewa zawadi wala kurithiwa.

[17] Kuzuia au kuuza maji ya ziada ambayo mtu hana matumizi yake ni jambo lisilokubaliwa kishariy’ah; vyovyote itakavyokuwa asili ya maji yale ni kisima au chemchem, katika ardhi anayoimiliki au katika ardhi ya mtu mwingine. Hata hivyo, maji yaliyohifadhiwa kwa matumizi binafsi yanaweza kuuzwa ni jambo linaloruhusiwa.

[18] Mapigo ya ngamia ni kumchukua ngamia dume na kumkodisha kwa mtu mwenye ngamia jike ili ampande.

[19] Kulikuwa na aina mbili za biashara hii. Aina ya mfano wa kwanza ni kununua kizazi cha mnyama ambaye bado hajazaliwa, nayo hufanyika kwa kulipa malipo kabla. Aina ya pili ni kumuuza mnyama kwa sharti la kuchukua mtoto atakayezaliwa. Aina zote za biashara hizi zilikatazwa kwa sababu ya mikataba yake kutokuwa wazi.

[20] Al-Walaa: mtumwa aliyeachwa huru akifa na kama hana wa kumrithi basi atarithiwa na yule aliyemuacha huru. Hadiyth imeweka wazi kuwa Al-Walaa ni kama uzawa wa mtu. Ikiwa kizazi cha mtu hakiwezi kuuzwa au mtu kupewa hiba, basi hivyo hivyo kuuza Walaa au kutoka kama zawadi ni jambo lililokatazwa.

[21] Biashara ya kurusha kijiwe ziko aina nyingi ikiwemo mmoja kumuambia mwengine: “Rusha kijiwe hiki, kitakapoangukia katika nguo yoyote itakuwa ni yako”, kwa kiasi kilichopangwa kabla. Biashara hii ni ya udanganyifu na ni biashara ya kubahatisha, kama vile kuuza njiwa akiwa hewani anaruka au kuuza samaki aliye baharini au kumuuza mtumwa aliyepotea au mnyama. Hizi ni aina za biashara zilizokuwa zama za ujahiliya.

[22] Katika sampuli hii ya biashara muuzaji anapanga bei mbili katika uzo moja. Uzo moja kwa malipo taslimu na lingine kwa mkopo. Bei ya mkopo linakuwa juu zaidi, fedha iliyozidi katika bei ya mkopo ni riba ambayo ni haramu.

[23] Baadhi ya Wanazuoni wa Hadiyth hawakubaliani na mapokezi haya ya mwisho ambayo Muhammad bin ‘Amr akiwa mmoja wa wapokezi. Hata hivyo imewekwa katika Hadiyth Hasan na wengine Swahiyh. Angalia ‘Irwaa Al-Ghaliyl, Shaykh Al-Albani 5/149-150.

[24] Biashara hii ina sampuli mbili: aina ya kwanza ni kama mtu anayeuza farasi kwa riyali mia moja kwa mkopo kwa sharti kuwa mnunuzi atalipa muda fulani. Ikiwa mnunuzi atashindwa kulipa deni lile kwa muda uliopangwa basi muuzaji atamnunua farasi yule kwa shilingi mia na hamsini na kumuacha mnunuzi akidaiwa shilingi mia na hamsini. Hii ni haramu. Sampuli ya pili ni mfano wa nyumba yenye thamani ya shilingi milioni kumi na mbili, huuzwa kwa mtu kwa milioni kumi kwa sharti kuwa mnunuzi atamuazima muuzaji shilingi milioni mbili.

[25] Kama vile kumuambia mtu: “Ntakuuzia nyumba hii kwa shilingi milioni kumi pesa taslimu au kwa shilingi milioni kumi na tatu kwa mkopo.”

[26] Kuuza kitu usichokimiliki mfano wake ni kama vile kuenda sehemu na ukanunua kitu na hapo hapo dukani ukamuuzia mtu na ukamlipa mwenye duka na faida uchukue wewe.

[27] ‘Urbaan ina maana ya kuweka kwa ajili ya kukilinda kitu au kukizuia kwa ajili ya kukinunua kitu. Kwa mfano kama mtu atatoa hela ya kununua mnyama kama hivi na mnunuzi anakaa na hela ile iliyowekwa kama dhamana, kama biashara itakamilika fedha zile zitakatwa katika mauzo. Mauzo haya si halali kulingana na Hadiyth. Hata hivyo, baadhi ya Wanazuoni wanazingatia Hadiyth hii kuwa ni dhaifu. Hivyo basi, imekuwa ni haramu kwa muono wa Imaam Maalik na Shaafiy’ na kukubaliwa na Imaam Ahmad. Fedha hizi ambazo mtu anazitoa ambazo hazitarejeshwa kwake kama biashara haijakamilika huitwa ‘dhamana isiyorejeshwa’.

[28] Ina maana kuwa mtu anaponunua bidhaa sehemu hairuhusiwi kuiuza pale pale tena, hadi itakapohamia katika miliki ya mnunuzi kabla ya kuiuza tena. Hukumu hii ni kwa bidhaa ambayo inaweza kuhamishika. Kwa biashara kama ya nyumba, inawezekana pale tu baada ya kukamilisha taratibu zote za mauzo, hapo naye anaweza kuiuza.

[29] Dirhamu ni sarafu ya fedha, dinari ni sarafu ya dhahabu. Kubadilisha dinari na dirhamu na kinyume chake ni halali madamu mabadilishano haya yatamalizika na kuhitimishwa kwa bei ya siku ile na kila mtu atapokea haki yake kwa ukamilifu. Hii inafahamika kama biashara ya kubadilisha fedha.

[30] An-Najsh ni mtu kuzidisha thamani ya bidhaa kwa kutokuwa na niyyah ya kununua, bali ili watu wainunue kwa bei ya juu.

[31] Muhaaqalah: ni kuuza nafaka katika shuke lake (kabla kuvunwa) kwa kukadiria na nafaka zilizopimwa (zilizovunwa) kama ngano.

[32] Muzaabanah: ni kuuza matunda (au mazao) yaliyo katika shamba (ambayo bado hayajachumwa) kwa matunda yaliyokwisha chumwa. Mauzo haya si halali

[33] Mukhaabarah: ni mtu kukodisha shamba ili malipo yake yawe ni baadhi ya mazao yatakayotoka kama ni nusu ya mazao au theluthi. Kimsingi mauzo haya ni halali na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliyafanya kwa Mayahudi wa Khaybar. Kinachokatazwa na Hadiyth hii ni kuainisha kipande cha mazao ya ardhi mmiliki na kipande kingine cha ardhi cha aliyekodishwa. Suala hili linaleta mgongano na wamiliki wa ardhi na wakodishaji, ikiwa mazao ya mwenye shamba yasipofanikiwa kuvunwa na ya mkodishaji kuvunwa au kinyume chake. Hata hivyo hakuna tatizo kama watakubaliana kushirikiana mazao yote yaliyovunwa kwa kiwango watakachobaliana.

[34] Thun-yaa ni kuuza mazao shambani yakiwa katika mti kwa bei kadhaa kwa sharti la kuvuna baadhi ya matunda. Hii ni haramu kwa kuwa kilichovunwa hakijulikani. Hata hivyo kama kiwango kitaainishwa basi inaruhusiwa.

[35] Mukhaadhwarah: ni kuuza nafaka au matunda kabla ya kuiva.

[36] Mulaamasah: ni mtu aiguse nguo bila ya kuitazama. Mauzo kwa bei iliyokwishapangwa anainunua akiwa amefunga macho au katika kiza kwa mguso mmoja wa mkono wake. Kwa mfano mtu anakwenda kwa muuza nguo na anapendekeza anunue jora ya kitambaa kwa kiasi cha fedha. Anakubali kununua kwa sharti la kuwa atafunga macho kisha atashika jora la kitambaa, na atanunua jora ambalo atashika mwanzo. Biashara ya sampuli hii imekatazwa.

[37] Munaabadhah: ni mtu kuirusha nguo yake katika hali ya kiza kwa mtu mwingine kabla ya kuikagua au kuitazama na huyo anayerushiwa huinunua.

[38] Jina lake kamili ni Abuu ‘Abdir-Rahmaan Twaawus bin Kisan Al-Faaris, ameachwa na wao (kina Al-Himyaar). Jina lake alikuwa ni Dhakwaan na Twaawus ilikuwa ni lakabu yake. Ni madhubuti, faqihi (Mwanachuoni wa Shariy’ah). Alikuwa ni Taabiy’ wa daraja la tatu. Amepokewa akisema: “Nimekutana na Maswahaba 50 katika uhai wangu.” Ibn ‘Abbaas amesema: “Sijawahi kumuona mfano wake.” Alifariki mwaka wa 106 Hijriyyah.

[39] Kuwapokea wasafiri nje ya mji, kwa lengo la kununua bidhaa kutoka kwao kwa bei ya chini, na kuwaficha hali halisi ya soko lilivyo ni jambo lisiloruhusiwa. Misafara iruhusiwe kufika katika vituo vyake vya biashara na kujua bei ya soko. Kabla ya hili kuuza na kununua hakutakiwi. Ikiwa mtu atapatana katika mauzo na baadae muuzaji akafahamu kuwa amedanganywa anaweza kuvunja biashara ile.

[40] Najsh imeelezwa hapo kabla. Maelezo mengine ni kuwa ikiwa mtu kanunua kutoka kwa mwenye duka, mwenye duka mwingine hatakiwi kumshawishi mtu yule anunue kutoka kwake kwa kumuuzia kwa bei ya chini zaidi.

[41] Haitakiwi kwa mwanamke kuleta na kusababisha chuki baina ya mke na mume, ili asababishe talaka baina yao ili apate kuolewa yeye na mme huyo. Hali kadhaalika ni haramu kumuoa  dada au ndugu ya mtu kwa sharti la kumuacha mke wake wa kwanza.

[42]  Kwa mfano mtu akikubaliana na mtu kumuuzia kitu kwa shilingi elfu moja. Hairuhusiwi kwa mtu mwingine kumshawishi muuzaji asiuze kwa shilingi elfu moja, kwa yeye kutaka kununua kwa elfu moja na mia tano kwa kitu kile kile. Hata hivyo ikiwa bidhaa imewekwa kwa ajili ya ushindani kama vile mnadani, inafaa mtu kuongeza thamani.

[43] Hadiyth hii inaashiria kufarakanisha haifai. Hadiyth hii inaweka wazi kama biashara hiyo itaendelea ni haki kuivunja.

[44] Hadiyth hii inaashiria kuwa suala la kupanga bei haliruhusiwi kwani inapelekea hasara wakati mwingine kwa wafanya biashara, kwa upande wa pili inapelekea katika janga la njaa. Mahitaji muhimu ya maisha yanakosekana na uchafu unaibuka katika jamii.

[45] Ma’mar bin ‘Abdillaah bin Naafi’ bin Nadla bin Harthaan Al-‘Adawi ni Swahaba mkubwa, ni miongoni mwa waliohajiri Uhabeshi. Hijra yake Madiynah ilichelewa.

[46] Ihtikaar – Ukiritimba ni kuzuia bidhaa kwa ajili ya mauzo ya faida kubwa zaidi baadae. Ukiritimba umekatazwa na ni haramu kwani inatengeneza uhaba wa mahitaji muhimu wa chakula wakati katika hali halisi vyakula vipo.

[47] Katika Hadiyth,  siku tatu zimetajwa kwa sababu kwa uchache siku tatu zinahitajika kutathmini kiasi halisi cha maziwa katika kiwele. Wakati mwingine nyasi kavu na kubadilika kwa sehemu husababisha maziwa kuongezeka. Ikiwa maziwa yataachawa katika kiwele kwa matumizi binafsi na si kwa kuuza inaruhusiwa. Kwa hali yoyote ile, kuyaacha maziwa katika kiwele cha mnyama humuumiza mnyama.

[48] Ina maana kama mnunuzi ataona ubaya wa muamala huu, anaweza kurudi baada ya siku tatu. Kama mauzo ni maziwa ya ng’ombe, yatarudishwa kwa pishi (sawa na 2.6 kg) kwa nafaka yoyote, sio lazima iwe tende.

[49] Hii ina maana kwamba udanganyifu ni jambo lililokatazwa. Maana ya Hadiyth hii ni Udanganyifu si laiki ya watu wangu. “Ni tabia ya kikafiri.” Haina maana kuwa yeye ni kafiri.

[50] Ni haramu kuuza zabibu kwa mtengeneza mvinyo. Kusaidia kitendo chochote cha ubaya na kwa malengo mabaya ni haramu. Qur-aan Suwrah Al-Maaidah (5: 2) inatuamrisha kufanya na kushirikiana kwa matendo mema na kutukataza kabisa kushirikiana na madhambi na matendo mabaya.

[51] Ina maana hadi wakati wa kurudisha bidhaa (kama haitakiwi) faida na hasara inakuwa kwa mnunuzi. Jaalia mauzo ni ya mnyama, na mnyama akafa katika muda walioahidiana arudishe basi hasara inakuwa kwa mnunuzi, hali kadhalika kama atamuuza kwa bei ya juu zaidi wakati ule faida ataichukua yule mnunuzi.

[52] Huyu ni Ibn Ja’ad au Ibn Abiy Ja’ad na inasemekana kuwa baba yake akiitwa ‘Iyyaad Al-Baariqiyy, ni sehemu ya ukoo wa Baniy ‘Azd ambaye ni Baariqiyy bin ‘Adi bin Haaritha. Alikuwa akiitwa Baariqiyy kwa sababu aliishi katika mlima ulioitwa Baariqiyy. ‘Urwah alikuwa ni Swahaba aliyemtumikia ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kama Qadhi wa mji wa Kufa, aliishi huko na Hadiyth zake nyingi zilipokewa na watu wa huko.

[53] Udhwhiyyah ni mnyama anayechinjwa katika siku ya ‘Iyd ya Hajj.

[54] Hadiyth hii inaweka wazi mambo manne: (i) Wakili anapewa nguvu na mamlaka ya kutumia utajiri wa mdhamini wake. (ii) Huwezi kuuza bidhaa ila kwa ridhaa ya mwenyewe. (iii) Kuwa ni ruhusa kumuuza mnyama wa Udhwhiyyah na kumnunua mwingine kwa badala, biashara hii haitakiwi iwe kwa ajili ya faida. Kama kutakuwepo na faida yoyote kutokana na biashara hii basi itolewe kama Swadaqah. (iv) Ya kwamba wema wowote ni lazima ushukuriwe na uwe na malipo yake.

[55] Chuchu la mnyama, yaani kiwele chake.

[56] Katika Hadiyth hii kumetajwa mambo sita yaliyokatazwa katika biashara na sababu zake zinatofautiana. Uharamu wa mawili yaliyotajwa hauna utata ndani yake kwani Wanazuoni wamekubaliana, nazo ni katika biashara za kubahatisha. La tatu ni haramu kwa sababu ya kutokuwa na hakika na hali ya mtumwa aliyekimbia. La nne ni haramu kwa kuwa haipo katika miliki, la sita ni haramu kwa kuwa hakuna uhakika kama mzamiaji atatoka na chochote anapozamia. Nayo ni hali ya kubahatisha. Kubahatisha kwa mpiga mbizi ni mtu kusema: “Nitapiga mbizi katika maji kwa shilingi kadhaa kitakachotoka ni chako.” Biashara hii imekatazwa kwa sababu ya udanganyifu.

[57] Kiwele: ziwa la mnyama. Katika Hadiyth hii aina tatu za biashara haramu zimetajwa. Ya kwanza ni matunda ambayo bado hayajawiva, matunda yaliyopo mtini kwani kuna uwezekano wa kuharibika hadi yawive. Nukta ya pili ni kuwa mti ni mali ya muuzaji na matunda yake ni mali ya mnunuzi. Ushirikiano wao wa muda mrefu hauwezi kudumu sana. Aina zingine za biashara zilizoharamishwa hapa ni Sufi ya kondoo mgongoni mwake kabla hajanyolewa na maziwa ya mnyama yakiwa katika kiwele chake. Hizi ni haramu kwa sababu kiwango cha sufi na maziwa hayajulikani, ni aina ya bahati nasibu ambayo ni biashara ya kubahatisha.

[58] Madhwaamiyn neno la kiarabu lenye maana ya kizazi kwa maana ya mimba ambayo haijazaliwa katika tumbo la mamake.

[59] Al-Malaaqiyh ni manii katika mgongo wa baba.

[60] Ikiwa wameshakubaliana kuwa mali inaweza kurudishwa, mnunuzi ana haki kamili ya kurejesha. Hata hivyo kama hawajakubaliana hapo kabla na mnunuzi anataka kurejesha, na akamrudishia muuzaji, basi yule muuzaji atakapokubali, kwa khiyari yake, kurudisha bidhaa ile, Allaah atamsamehe madhambi yake.

 

 

Share