01-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Utangulizi

 

 

Kwa Ajili ya Allaah ... Kisha Kwa Ajili Ya Historia:

 

01-Utangulizi

 

 

Sifa njema zinamstahiki  Mwenyezi Mungu mlezi wa viumbe na tunamtakia rehema na amani Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yeye na ahli zake na sahaba zake.

 

  Ama baada ya salaam

 

Tulikua katika jumuiya ya Swalahuddiin tukizungumzia haja ya kuwa na kitabu chenye ufupi wa maelezo ya msingi wa shi’a (Ithna ashariya) kwa sharti waweze kufaidika kwa kitabu hicho watu  wa kawaida na watu maalum. Pindi tulipo kuwa tunatafuta nani aandike kitabu hicho miongoni mwa wanazuoni na wenye  ujuzi na waliobobea kikatufikia kitabu hiki : -

 

 

(KWA AJILI YA ALLAAH… KISHA KWA AJILI YA HISTORIA) kilicho tungwa na ASSAYED HUSSEIN AL MUSAWIY, miongoni mwa wanazuoni wa najaf na baada ya kukisoma tukaona kinakidhi  lengo na ziada, ama ziada tunayoikusudia hapa ni mtungaji wa kitabu hicho kwa vile anazingatiwa ni mwanazuoni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa shia.na kwa sababu ya kusoma kwake na kufundisha kwake katika sehemu kuu (Vyuo vikuu)  za Najaf. Na  alikuwa na mahusiano makubwa na wanazuoni na Ma,aayaati wa kishia kwa mfano: Kashif Alghataa, Alkhuuiy, Al-Sadir, Al-Khamenii,na Abdul Hussein Sharafuddin, ambaye alikuwa anakuja sana katika mji wa Najaf, achilia mbali hili na lile, baba yake mtungaji pia alikuwa mwanachuoni katika wanachuoni wakishia.

 

 

 Mtungaji amezungumzia katika kitabu chake maajabu aliyoyakuta na uzoefu wake katika rejea ya vitabu vya mashia  kwa njia nzuri yenye kuvutia na yenye ufupi na baada ya kutaja yaliokuwa yakimtokea akiwa pamoja nao  (wanachuoni wa kishia) au akiwa na mmoja wao huwarejesha wasomaji wake katika vitabu vyao mama ambavyo vinaonyesha ruhusa ya kitendo hicho kiovu.

 

 Na yeyote atakayechukuwa kitabu hiki na kukisoma kwa utulivu basi atauona ukweli wa mtungaji. (wala hatumtakasi mtu mbele ya Allaah) na ataona tofauti ya njia alizozitumia kinyume na wenzake miongoni mwa watungaji wa kishia ambao wanaokosoa  baadhi ya misingi  ya dhehebu lao,  Mungu  amjaze kila la kheri kwa kitabu chake hiki kizuri , na amuepushie shari ya wenye chuki naTumesikia kwamba wanampangia njama Na ndio maana hakuweka  jina lake kwa uwazi zaidi ili asijulikane na kamkuta ya sio mema (soma ukurasa wa 91) katika kitabu hiki.

 

 

Tuna muomba Mwenyezi Mungu ajaalie amali zetu ziwe kwa  kwa ajili ya kupata radhi zake tukufu.

 

JUMUIYA YA SWALAHUDDIN,

14, SAFAR 1422.

 

       Sifa njema zinamstahiki Allaah mlezi wa viumbe na rehema na amani zimshukie mjumbe wetu muaminifu na Aali zake wema watakatifu na wafuasi wao kwa mazuri mpaka siku ya kiyama.

    

 

      Ama baada ya hayo, hakika muislamu anajua kuwa uhai unakwisha kwa mauti kisha inaamuliwa hatima yake ama kwenda peponi au motoni. Na bila shaka kuwa muislamu ni mwenye kupupia ili awe miongoni mwa watu wa peponi. Kwa ajili  hiyo lazima afanye amali   yenye kumridhisha mola wake mtukufu na ajiweke mbali na makatazo yake, mambo yanayo muingiza mtu katika ghadhabu za Allaah  kisha adhabu yake. Kwa ajili hiyo tunamuona muislamu anakuwa na pupa katika kumtii mola wake, na huo ndio mwendo wa muislamu wa kawaida, seuze watu maalum (wenye elimu)?

 

    

   Hakika uhai kama inavyojulikana una njia  nyingi na udanganyifu mwingi,mwenye akili ni yule anayefuata njia inayomfikisha peponi hata kama ni ngumu na kuacha njia inayomfikisha motoni hatakama ni nyepesi  sana.

     

       Riwaya hii  nimeiweka  kwa mtindo wa utafiti (bahthi) ambayo nimeitamka kwa ulimi wangu na  kuiandika kwa mkono wangu , nimekusudia kwa kazi hii kupata radhi za Allaah na kuwanufaisha ndugu zangu madamu nipo hai kabla sijavikwa sanda.

 

    Nimezaliwa  Karbala na nikaleleka katika mazingira ya kishia  chini ya uangalizi wa baba yangu mfuasi mzuri wa dini. Nimesoma katika shule za mji huo(karbalaa) mpaka nimekuwa kijana baro baro na akanipeleka baba yangu kwenye vyuo vya elimu vya Najaf mama wa vyuo vya duniani ili nichote elimu kwa mabingwa wa maulamaa mashuhuri katika zama hizi kwa mfano: -

 

  Al-imam Assayed Mohamed Al-hussein (kashif  Al-ghatwaa).

 

Tulisoma  katika madrasa za Najaf za elimu za juu ikawa matamanio yangu ifikie siku ambayo nitakuwa marejeo katika mambo ya dini  siku ambayo nitakuwa kiongozi wa moja ya vyuo vikuu ili niweze kuihudumia dini yangu na umma wangu na kuwaendeleza waislamu.  

  

 

      Na  nilikuwa nikitamani kuona waislam ni Umma mmoja, na taifa moja wakiongozwa na imam mmoja, na katika wakati huohuo nikitamani kuona mataifa ya kikafiri yakiporomoka na kuanguka mbele ya umma wa kiislam. Na kuna matarajio mengi zaidi ambayo kila kijana muislam mwenye uchungu na dini yake huyataraji. Na nilikuwa nikijiuliza ni kitu gani kilicho tupelekea katika hali hii ya udhalili  tukonyuma kimaendeleo tumesambaratika tumefarikiana? Na nilikuwa  nikijiuliza vitu vingine vingi  vinavyopita katika fikra zangu  kama inavyo pita katika fikra za kila kijana muislam, lakini sipati majibu ya maswali yangu.

  

   

        Akanisahilishia mwenyezi mungu kujiunga na masomo, na kutafuta elimu, katika kipindi cha masomo zilikua zinanipitia hoja zinazo nifanya nisimame nitafakari, na mambo tofauti yanayoshughulisha moyo wangu na matukio yanayonishangaza , lakini nilikua naituhumu nafsi yangu kwa kuelewa vibaya, na uchache wa ufahamu, nikajaribu kuyaweka mambo hayo  mbele ya mmoja wa viongozi na waalimu wa vitengo vya elimu ya dini; Na alikua mtu mwerevu alijua jinsi ya kuyatatua mas’ala hayo basi  akataka ayazime katika uchanga wake kwa maneno mepesi akaanza kuniuliza: Unajifunza nini katika kitengo cha elimu?

 

Nikajibu: Madh-habu ya Ahlil- bait.

Akaniuliza, Je una mashaka na madh-habu Ahlul-bait?

Nikamjibu kwa ukakamavu, mwenyezi mungu apishie mbali.

 

Akasema ondoa wasiwasi huu katika nafsi yako, Hakika wewe ni mfuasi wa Ahlil-baiti wao wamepokea kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, na Muhammad amepokea kutoka kwa mwenyezi mungu mtukufu.

     

     Nilinyamaza kidogo mpaka nafsi yangu ikatulia, kisha nikamwambia:- Mwenyezi mungu akubariki kwa kunitibu na wasiwasi huu, kisha nikarudi katika masomo yangu na yakanirudia Maswali yale na maulizo na kila nilipokua  nikipiga hatuwa katika masomo yalikua yakiongezeka maswali, na kuongezeka kasoro ninazo zigunduwa.

 

 

La msingi ni kuwa nilimaliza masomo yangu kwa mafanikio makubwa,na nikapata shahada yangu ya kwanza ya katika daraja la “Ijtihaad” kutoka kwa mwanazuoni pekee zama hizo Mheshimiwa mkuu wa chuo Muhammad Al Hussain Al Kashif lgahtaa mkuu wa chuo,na baada ya hapo nilianza kufikiri kwa kina zaidi juu ya mas’ala haya,sisi tunasomea madhab ya Ahlulbait (AS) tunasomea masuala ya sheria ili tumuabudu mwenyezimungu kwazo,lakini ndani yake kuna vipengele vya wazi kabisa vinavyomkufuru mwenyezimungu mtukufu.

Ee mola wangu,ni mambo gani haya tunayoyasoma?! Je yanaweza yakawa haya ndio madhab ya Ahlul bait kweli?! Hakika hili humsababishia mtu ugonjwa wa nafsi katika shaksia yake,ni vipi atamuabudu mwenyezimungu hali yakuwa anamkufuru?!.

 

Vipi atawafuata Ahlul bait,atawapenda na atasoma madhab yao hali ya kuwa anawatukana?!

       

         

      Kutokana na rehema zako mola wangu, na upole wako kwangu kama zisinge nidiriki rehema zako ningelikua miongoni mwa waliopotea , bali miongoni mwa waliopata hasara. Na ninarudi kuiuliza nafsi yangu,Ni nini msimamo wa viongozi na maimamu hawa na kila ambao walio tangulia  katika mafahali wa wanazuoni. Nini msimamo wao katika jambo hili? Je hawa kuwa wameliona hili ambalo nililo lisoma?! Naam, bali miongoni mwa vitabu hivi wengi wao ndio walio vitunga, na yaliyomo ndani yake yameandikwa kwa kalamu zao basi likawa jambo hili linatonesha moyo wangu, na inauongeza uchungu na majuto.

 

            

    Nilikuwa na haja ya kumpata mtu wa kumshitakia huzuni zangu, na  wakumtolea masikitiko yangu,

 

 

 Mwisho nikaongozwa kwenye fikra nzuri zaidi nayo ni kusoma  kwa upana zaidi  na kuuangalia upya  mtazamo  wa mada zangu za kielimu, Basi  nikaanza kusoma kila kilichopo katika marejeo yenye uhakika na hata vile visivyo vya uhakika, basi nilisoma kila kitabu kilichopo  mbele ya mikono yangu, ikawa  zinanisimamisha baadhi ya ibara na hoja ambazo nilihisi kuna  haja ya kuziwekea Taaliiq,(maelezo) basi nikawa nazinakili hoja hizo na kuzitolea maelezo kwa yanayo pita katika nafsi yangu,  pindi nilipo maliza kusoma marejeo ya uhakika, Nikajikuta ndani ya rundo la vipande vya karatasi, Nikavihifadhi kwa matarajio kwamba itafika siku mwenyezimungu aktahukumu lifanyike jambo ambalo ameliandika.

 

    

     Na uhusiano wangu ukabaki kuwa mzuri pamoja na kila marejeo(maulamaa) ya kidini, na wanazuoni na viongozi ambao nilikutana nao, Na nilikuwa nachanganyika nao ili niweze kufikia kwenye lengo  ambalo litanisaidia pindi siku nitakayochukua uamuzi mzito, Nikasimama katika mas’ala mengi mpaka kukinai kwangu kukawa kumekamilika katika kuchukua uamuzi mzito, lakini nikawa nasubiri wakati na nafasi muafaka.

 

 

     Na nikawa namuangalia rafiki yangu msomi mwanazuoni (Musa Almuusawi) Nikamuona ni  mfano mzuri(wa kuigwa) wakati alipotangaza kupinga upotofu uliojitokeza katika mfumo wa kishia na kujaribu kwake kwa juhudi kwa juhudi kubwa  kusahihisha mfumo huu.

 

 

     Kisha kikatolewa kitabu na  bwana Ahmadu Alkaatibu (maendeleo ya fikra yakishia), Na baada ya kukisoma nikaona hakika umefika wakati wangu katika kusema ukweli, Nakuwafafanulia ndugu zangu waliohadaiwa, kwa sababu sisi kama wanazuoni ni wenye kuulizwa juu yao siku ya kiyama. Basi hatuna budi (nilazima) kuwafahamishe ukweli ujapokua mchungu. Na huenda njia niliyoitumia inatofautiana na njia waliyoitumia mabwana wawili: Almusawwi na Alkaatib, katika matokeo ya utafiti wa kielimu, hii inatokana na sababu ya yale aliyoyapata kila mmoja kati yetu katika kipindi cha utafiti wake alioufanya.

 

 

     Na huenda mabwana hao wawili waliotajwa hali yao inatofautiana na hali yangu, imekuwa hivyo kwani kila mmoja kati yao amehama Irak, na kuishi  katika nchi miongoni mwa nchi za magharibi, na huko ndio wameanza kazi zao.

 

     Ama mimi bado nipo ndani ya Irak , tena ndani ya Annajaf yenyewe. Na vitendea kazi nilivyo kuwa navyo haviwezi kufikia ngazi ya vitendea kazi walivyo kuwa navyo mabwana wawili hao. 

 

 

     Kwani mimi baada ya kufikiri sana kuhusu kubaki hapa(Irak) au kuondoka! Nikaamua kubaki na kufanya kazi hapa hapa(Anajaf) nikusubiri na kutarajia malipo kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Nami nikiwa na yakini kuwa kuna mabwana wengi wanaohisi kusononeka na kusutwa  nadhamira zao kwa kunyamaza  kwao na kuridhia kwao yale wanayoyaona na kuyashuhudia, na kwa yale wanayoyasoma katika vitabu vikubwa ambavyo wanavyo,basi ninamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) akijaalie kitabu changu kiwe chenye kutoa msukumo kwao katika kujirudi.Na kuacha njia ya upotevu na kufuata njia ya haki,kwani umri ni mfupi,na hoja imesimama juu yao,hawatabaki na sababu baada ya hapo.

 

 

   Na kuna mabwana wengine  ambao nina uhusiano nao walikubali mwito wangu  (namshukuru Allaah)  waliuona ukweli huu ambao niliufikia katika utafiti wangu na wao wakaanza kuwalingania watu wengine tunamuomba mwenyezi mungu atuwafikishe sisi na wao kwa kuwaonyesha watu ukweli na kuwatahadharisha kutumbukia katika batili (upotevu) hakika yeye ndie mkarimu zaidi kuliko wote wenye kuombwa.

 

 

     Nami nina fahamu vyema kitabu changa hiki kitapuuzwa na nakukadhibishwa na kutupiwa tuhuma nyingi za uongo na batili, na jambo hili halitanidhuru kwani nimayaweka hayo yote katika malipo yangu. Na ninafahamu watanituhumu mimi ni kibaraka wa Israel au Amerika au watanituhumu kwamba nimeuza dini yangu na dhamira yangu kwa malipo ya Dunia, na Jambo hili halipo mbali na wala si geni,kwani alishatuhumiwa rafiki yetu mwanachuoni  Musa  Al-muusawi,kwa tuhuma mfano wa hizi. Ikafikia hata bwana Ally Al-gharwiyy,kusema kwamba mfalme wa Saudia Fahad bin Abdulaziz amemhadaa Dr.Al-muusawy kwa mwanamke mzuri  katika ukoo wa Al-Saud, na kumfanya mzito kifedha, na kumuekea kiwango kikubwa cha fedha katika benki za Amerika. Kwa kuingia katika madh-habi ya Al waahabiya!!

 

 

     Ikiwa hapa ndipo alipo fikishwa  Dr. Al-muusawy  kwa kusingiziwa uongo na uvumi usio kuwa na msingi wowote, je mimi nitafikishwa wapi? Na watanisingizia mabaya gani? Na huenda wao wananitafuta ili waniue, kama walivyowaua waliosema ukweli kabla yangu.Walimuua mtoto wa maulana , AAYATULLAHI AL-UDHMAA AL-IMAM ASSAYYID ABIL HASSAN AL-ASFAHANIY kiongozi mkuu wa shia  katika zama za ghaibu kuu hadi sasa,(shia wanaitikadi yakuwa kuna imamu wao alie potea na atarudi siku yoyote ndio hiyo wanayoiita ghaibu kuu) na bwana mkubwa wa wanachuoni wa kishia  bila kupingwa wakati alipotaka kuusahihisha mfumo wa kishia, na kuutoa uzushi ulioingizwa, jambo hilo halikuwapendezea, wakamchinja mtoto wake kama achinjwavyo kondoo ili wamzuie kiongozi huyo na mpango wake wakuusahihisha dosari na upotevu wa kishia,kama walivyo muua bwana AHMAD AL-KASRAWIY,wakati alipo tangaza kujivua katika upotevu huu,nakutaka kuusahihisha mfumo wa kishia, basi wakamkata kata kiungo kimoja kimoja.

 

 

     Na kuna wengi waliofikia mwisho huu kutokana na kupinga kwao imani hiyo potofu ambayo imeingizwa katika ushia, kwa hiyo si ajabu kunitakia mimi uovo kama huo,

 

 

     Haya yote hayanishughulishi,na inanitosha kusema ukweli na kuwanasihi ndugu zangu na kuwakumbusha  na kuigeuza mitazamo yao waifuate haki. Na lau ningekua nataka chochote katika starehe za dunia,kwa hakika Mut’aa  na khumus zingenitosha kwa kunitekelezea hilo,kama wengine wafanyavo, mpaka wakawa matajiri wa mji , na baadhi yao wanapanda magari yaliyo bora zaidi kwa kila toleo jipya,

 

 

     Lakini mimi ninamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) nimeyatupilia mbali haya yote tangu nilipo ujua ukweli,nami hivi sasa ninapata riziki yangu na familia yangu kwa kazi za biashara halali na nimegusia katika kitabu hiki muudhui maalumu ili ndugu zangu waione haki kiasi ambacho usibaki ukungu machoni  mwa yeyote kati yao.

 

 

     Na nina nia ya kuandika vitabu vingi vinavyohusu maudhui nyinginezo, ili waislamu wote wawe katika ubainifu,usibakie udhuru kwa mwenye kughafilika au kuwa na hoja jahili. Nami nina yakini kuwa kitabu changu hiki kita kubaliwa na wale wote wanaoutafuta ukweli na haki, nao ndio wengi zaidi,na nina mshukuru Allaah kwa hilo na ama yule atakae khiyari kubaki katika upotevu ili ukuu wao usipotee na kupoteza mut’aa na khumusi miongoni mwa wale waliovaa vilemba, na kupanda magariaina ya Mercesdes na Subaru hawa hatuna maneno nao, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ndie tosha yao  juu ya yale waliyoyafanya na wanayoendelea kuyafanya  katika siku ambayo hayatamfaa mtu mali wala watoto isipokua atakae fika kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hali ya kuwa moyo wake umesalimika.

 

 

     Na nina mshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)ambae ametuongoza katika dini hii tusingekua  tumeongoka kama   Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) asingetuongoza.

 

 

Share