32-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Allaahumma ‘Aafiniy Fiy Badaniy… Laa Ilaaha Illa Anta – Miongoni Mwa Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

 

32-Allaahumma ‘Aafiniy Fiy Badaniy… Laa Ilaaha Illa Anta – Miongoni Mwa Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni

 

 

عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبِي بَكْرَةَ، أَنَّهُ قَالَ لأَبِيهِ يَا أَبَةِ إِنِّي أَسْمَعُكَ تَدْعُو كُلَّ غَدَاةٍ: ((اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَدَنِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي سَمْعِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَصَرِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ)) تُعِيدُهَا ثَلاَثًا حِينَ تُصْبِحُ وَثَلاَثًا حِينَ تُمْسِي‏.‏ فَقَالَ إِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدْعُو بِهِنَّ فَأَنَا أُحِبُّ أَنْ أَسْتَنَّ بِسُنَّتِهِ ‏

 

Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakrah (رضي الله عنه) ambaye amesema kuwa alimwambia baba yake: “Ee baba yangu, mimi nakusikia ukiomba hivi kila asubuhi:

 

اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَدَنِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي سَمْعِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَصَرِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ

 

Allaahumma ‘aafiniy fiy badaniy, Allaahumma ‘aafiniy fiy sam-’iy, Allaahumma ‘aafiniy fiy baswariy, laa ilaaha illaa Anta. Allaahumma inniy a’uwdhu bika minalkufri walfaqri. Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ‘adhaabil qabri laa ilaaha illaa Anta. (mara 3)

 

Ee Allaah, nipe ‘aafiyah (afya, siha, usalama, amani) ya mwili wangu, Ee Allaah, nipe ‘aafiyah ya masikio yangu, Ee Allaah, nipe ‘aafiyah macho yangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najikinga Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe)) Unaomba mara tatu asubuhi na jioni.  Akasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akitamka maneno hayo katika kuomba du’aa basi nami napenda kufuata Sunnah yake.” [Abuu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [22], Ibn As-Sunniy [69], Al-Bukhaariy katika Adab Al-Mufrad na isnadi yake ameipa daraja ya Hasan Al-‘Allaamah Ibn Baaz (رحمه الله) katika Tuhfat Al-Akhyaaar (Uk. 26). Pia Swahiyh Abiy Daawuwd (5090).]

 

 

Share