22-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Al-Wadiy’ah (Kuweka Amana)

 

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ اَلْوَدِيعَةِ

22-Mlango Wa Al-Wadiy’ah (Kuweka Amana)

 

 

 

 

 

 

823.

عَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ ، عَنْ أَبِيهِ ، عَنْ جَدِّهِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {مَنْ أُودِعَ وَدِيعَةً، فَلَيْسَ عَلَيْهِ ضَمَانٌ} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَهْ، وَإِسْنَادُهُ ضَعِيفٌ.

وَبَابُ قَسْمِ اَلصَّدَقَاتِ تَقَدَّمَ فِي آخِرِ اَلزَّكَاةِ .

وَبَابُ قَسْمِ اَلْفَيْءِ وَالْغَنِيمَةِ يَأْتِي عَقِبَ اَلْجِهَادِ إِنْ شَاءَ اَللَّهُ تَعَالَى.

Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb naye kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuwekewa amana hana dhamana.”[1] [Imetolewa na Ibn Maajah na Isnaad yake ni dhaifu]

Mlango wa kugawa Zakaah umetangulia katika mwisho wa “Kitabu cha Zakaah.”.

Mlango wa kugawa Fay na Ghaniymah utakuja baada ya “Kitabu cha Jihaad” In Shaa  Allaah

 

 

[1] Tofauti kati ya amaanah (amana) na ‘aariyah (mkopo) ni kuwa pale mtu anapoazima kwa ajili yake inakuwa ni ‘aariyah wakati amana ni ile mali mtu anayoiacha kwa mtu mwingine amuwekee. Mtu anaweza kutumia mali ya ‘aariyah kwa kuazima na kutumia lakini mali ya amaanah hairuhusiwi. Ikiwa ‘aariyah imeharibika na kupotea, aliyeazima itabidi alipe. Ama kuhusu mali ya amaanah ikiwa imeharibika au kuangamia kwa ajali, hatakiwi kulipa aliyewekewa dhamana, hata hivyo ikiwa mali ya amaanah imetumika au sehemu katika mali ile itabidi ailipe aliyekabidhiwa amaanah ile.

Share