01-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kiumbe Bora Kabisa Wa Kwanza Kufufuliwa Na Kwanza Kuomba Ash-Shafaa’ah

 

Fadhila Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

01-Kiumbe Bora Kabisa Wa Kwanza Kufufuliwa

Na Kwanza Kuomba Ash-Shafaa’ah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kiumbe bora kabisa, na wa kwanza kufufuliwa na wa kwanza atakayeruhusiwa kuomba Ash-Shafaa’ah (uombezi) Siku ya Qiyaamah:

 

عن أَبُي هُرَيْرَةَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَنَا سَيِّدُ وَلَدِ آدَمَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَوَّلُ مَنْ يَنْشَقُّ عَنْهُ الْقَبْرُ وَأَوَّلُ شَافِعٍ وَأَوَّلُ مُشَفَّعٍ " رواه مسلم  

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: ((Mimi ni Bwana wa mtoto wa Aadam Siku ya Qiyaamah, na (mimi) wa kwanza ambaye kaburi lake litapasuka, na wa kwanza wa kushufai, na wa kwanza ambaye atakayeombewa Ash-Shafaa’ah)) [Muslim]

 

An-Nawawiy akasema katika Sharh Swahiyh Muslim: “Hadiyth hii ni dalili ya ubora wake Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam juu ya viumbe wote wengineo kwa sababu madhehebu ya Ahlus-Sunnah wanawafikiana kwamba bin Aadam ni bora kuliko Malaika, naye Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam ni bora kuliko bin Aadam wengineo.”

 

 

Share