11-Zawadi Kwa Wanandoa: Kutangaza Ndoa

 

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

11-Kutangaza Ndoa

 

إعلان الزواج

 

 

Inapendeza kutangaza ndoa kishari'ah kwa kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :

أعلنوا هذا النّكاح , واجعلوه في المساجد

“Tangazeni ndoa hii, na ifanyeni Msikitini.”  (At-Tirmidhiy na Ahmad)

 

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema tena:

 

فصل ما بين الحلال والحرام الدّفّ والصّوت

“Mpaka wa baina ya halali na haramu ni dufu na sauti.” (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)

 

 

Na inawezekana kutangaza ndoa Msikitini kwa sharti ya kuwa mas-alah ya kuimba na dufu yawe nje ya Msikiti ili kuchunga adabu za Msikiti. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alikuwa akichukia sana ndoa kufanywa siri hadi ipigwe dufu na isemwe: “Tumewajia tumewajia, tusalimieni nasi tuwasalimie.” (Ahmad)

 

 

Na si vibaya kusheherekea ndoa kwa kuimba kwa lengo la kuzichangamsha nafsi, kwa sharti kuwa nyimbo hizo ziwe zimeepukana na matusi na uchafu wa maana mbaya na pia ni lazima ziwe nzuri zisiwe zenye kuhamasisha matamanio na kuwatoa watu haya.

 

 

Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  alisherehekea harusi ya al-Farigha bint Asad na akamsindikiza hadi kwenye nyumba ya mume wake, Nabiit bin Jaabir al-Answariy. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akauliza kumuuliza bibi 'Aaishah:

 

يا عائشة , ما كان معكم لهو؟ فإنّ الأنصار يعجبهم اللّهو

“Ee 'Aaishah, je, hamkuwa na Lahwu (kucheza na kujipumbaza)?! Kwani Answaar huvutiwa na Lahwu.” (Al-Bukhaariy)

 

 

Hali kadhalika imepokewa na bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  amesema: “Hukumfanyia fulani-kwa mayatima waliokuwepo kwake.” nikajibu: tumempeleka kwa mumewe, akasema: “Je, mlikwenda pamoja na kijakazi akapiga dufu na kuimba”, bibi Aisha akasema  aseme nini? Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema: “Aseme:

 

أتيناكم    أتيناكم            فحّيونا  نحيّيكم

 

ولولا الذّهب الأحمر          ما حلّت بواديكم

 

ولولا الحنطة السّمرا      ما سمنت عذاريكم

 

Tumewajia tumewajia,

 

Tusalimieni tuwasalimie

 

Na kama si dhahabu nyekundu

 

Msingeacha vijiji vyenu

 

Na kama si ngano nyeusi              

 

Basi wasingenenepa binti zenu

 

 

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik amesema: “Alipita Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  mwanzoni mwa kuhamia kwake Madiynah akiwa na harusi pamoja na wanawake, na mmoja wao alikuwa akisema:

 

Na akazawadiwa Kondoo              akipiga ukelele mkubwa kabisa

Na mumeo yupo Shamba               na unajua ya kesho.

 

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema:  “Usiseme hivyo bali sema:

 

أتيناكم    أتيناكم            فحّيونا  نحيّيكم

 

Tumewajia tumewajia,  Tusalimieni tuwasalimie

 

 

 

 

Share