21-Zawadi Kwa Wanandoa: Adabu Za Mtu Na Ndugu Za Mke Wake

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

21-Adabu Za Mtu Na Ndugu Za Mke Wake

 

أدب الرّجل مع أقارب زوجته

 

Katika jumla ya adabu ya mtu na ndugu za mke wake ni kutokutaja maneno au kufanya vitendo vya aina yoyote ile vyenye kuashiria mapenzi ya chumbani kama kubusu na mfano wa hayo, na hii ni katika adabu ya kuishi nao. Imepokewa kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: nilikuwa ni mtu mudhaa-a, nikiona haya kumuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa nafasi ya mtoto wake kwangu, nikamuomba Miqdaad aniulizie.

Share