41-Zawadi Kwa Wanandoa: Kumsaidia Mke Katika Kazi Za Nyumbani

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

41-Kumsaidia Mke Katika Kazi Za Nyumbani

 

مساعدة الزّوجة في الأعمال المنزلي

 

 

Amesema bibi 'Aaishah (Radhiya AAllaahu 'anha) :

 

قالت عائشة رضي الله عنها : كان صلى الله عليه وسلم يكون في مهنة أهله فإذا حضرت الصّلاة خرج إلى الصّلاة.

“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akiwasaidia katika kazi za nyumbani na inapowadia muda wa Swalah alikuwa akitoka kwenda kuswali.”

 (Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy na Ahmad)

 

Na alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), “Akitoa uchafu katika nguo zake, na akikama mbuzi maziwa na akijuhudumia mwenyewe.” (Ahmad)

“Na alikuwa yeye Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akishona nguo zake na kusafisha ndala zake.” (Ahmad)

 

Katika haya yote tunajifunza kutojikweza na tunahamasishwa kuwa na tabia nzuri za kusaidia katika kutunza nyumba na familia.

 

 

Share