Shaykh 'Abdul-'Aziyz Aal-Shaykh: Wanawake Kuvaa Mavazi Yenye Kubana

 

Wanawake Kuvaa Mavazi Yenye Kubana

 

Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Aal Shaykh

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Kuna wanawake wanaovaa sketi (skirts) na blauzi (blouses) ambazo zinawabana japokuwa hazionyeshi mwili au si fupi. Nini hukmu yake? Na unawanasihi nini wanawake hawa?

 

 

JIBU:

 

Mwanamke inampasa amwogope Allaah kuhusiana na mavazi yake, na kwamba avae mavazi ya kumsitiri vizuri na kwamba mavazi yake yasiwe ya kuonyesha mwili au ya kujishaua. Ikiwa anatoka nje hadharani au akiwa katika mikusanyiko ya wanawake wenzake kwa sababu huenda akapatwa na jicho baya si tu kutoka kwa wale ambao wana wivu naye bali hata wale ambao wana niyyah chafu kwake.

Kwa hiyo, kujifunika mavazi mazuri na kujisitiri ni katika yatakayompa heshima na kumhifadhi. 

 

 

[mufti.af.org.sa/ar]

 

 

Share