12-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amefunguliwa Kifua Chake Kuoshwa Kwa Zamzam Na Kujazwa Hikma Na Iymaan

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

12-Amefunguliwa Kifua Chake Kuoshwa Kwa Zamzam Na Kujazwa Hikma Na Iymaan 

 

www.alhidaaya.com

 

 

أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ كَانَ أَبُو ذَرٍّ رضى الله عنه يُحَدِّثُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((فُرِجَ سَقْفِي وَأَنَا بِمَكَّةَ، فَنَزَلَ جِبْرِيلُ  عَلَيْهِ السَّلاَمُ   فَفَرَجَ صَدْرِي، ثُمَّ غَسَلَهُ بِمَاءِ زَمْزَمَ، ثُمَّ جَاءَ بِطَسْتٍ مِنْ ذَهَبٍ مُمْتَلِئٍ حِكْمَةً وَإِيمَانًا، فَأَفْرَغَهَا فِي صَدْرِي، ثُمَّ أَطْبَقَهُ، ثُمَّ أَخَذَ بِيَدِي فَعَرَجَ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا‏.‏ قَالَ جِبْرِيلُ لِخَازِنِ السَّمَاءِ الدُّنْيَا: افْتَحْ‏.‏ قَالَ: مَنْ هَذَا؟  قَالَ: جِبْرِيلُ))

Imepokelewa kutoka kwa Anas kwamba Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Paa la nyumba yangu lilifunguliwa nilipokuwa Makkah (usiku wa Israa wal-Mi’raaj) akateremka Jibriyl (‘alayhis-salaam) akafungua kifua changu kisha akakiosha kwa maji ya Zamzam. Kisha akaleta chombo cha dhahabu kilichojaa Hikmah na Iymaan  akamwaga ndani ya kifua changu kisha akikufnga.  Kisha akanikamata mkono wangu  akapanda mbingu ya dunia (ya karibu).  Jibrily akamwambia Mlinzi wa mbingu ya dunia afungue mlango.  Mlinzi akasema “Nani?” Akajibu:  “Jibriyl.” [Al-Bukhaariy] 

 

Pia:

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَتَاهُ جِبْرِيلُ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يَلْعَبُ مَعَ الْغِلْمَانِ فَأَخَذَهُ فَصَرَعَهُ فَشَقَّ عَنْ قَلْبِهِ فَاسْتَخْرَجَ الْقَلْبَ فَاسْتَخْرَجَ مِنْهُ عَلَقَةً فَقَالَ هَذَا حَظُّ الشَّيْطَانِ مِنْكَ ‏.‏ ثُمَّ غَسَلَهُ فِي طَسْتٍ مِنْ ذَهَبٍ بِمَاءِ زَمْزَمَ ثُمَّ لأَمَهُ ثُمَّ أَعَادَهُ فِي مَكَانِهِ وَجَاءَ الْغِلْمَانُ يَسْعَوْنَ إِلَى أُمِّهِ - يَعْنِي ظِئْرَهُ - فَقَالُوا إِنَّ مُحَمَّدًا قَدْ قُتِلَ ‏.‏ فَاسْتَقْبَلُوهُ وَهُوَ مُنْتَقَعُ اللَّوْنِ ‏.‏ قَالَ أَنَسٌ وَقَدْ كُنْتُ أَرَى أَثَرَ ذَلِكَ الْمِخْيَطِ فِي صَدْرِهِ ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik kwamba  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akicheza na watoto wenzake alijiwa na Jibriyl (‘alayhis-salaam), akamchukua na kumlaza chini, kisha akampasua kifua chake na kuutoa nje moyo wake na kutoa kutoka ndani ya moyo huo kipande cha damu iliyoganda akasema: “Hicho ni kipande cha shaytwaan mwako.”  Kisha akauosha kwa maji ya Zamzam yaliyokuwemo ndani ya chombo cha dhahabu, kisha akaurudisha moyo mahali pake. Watoto waliokuwa wakicheza pamoja naye walikimbia mpaka nyumbani kwa mama yake yaani mnyonyeshaji wake (Bibi Haliymah As-Sa’diyyah), wakasema: “Muhammad keshauliwa!” Wakamkimbilia wakamkuta   (amekaa mzima hana chochote isipokuwa) rangi ya uso wake ilikuwa imebadilika na kugeuka (nyeupe).  Anas akasema: “Mimi mwenyewe niliona alama za mishono (ya sindano) katika kifua chake.”  [Muslim]

 

Share