Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwanamke Kupeana Mikono Na Wanaume Ajnabiy Akiwa Amevaa Glavu Mikononi

 

Mwanamke Kupeana Mikono Na Wanaume Ajnabiy Akiwa Amevaa Glavu Mikononi

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

 

www.alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Nini hukumu ya kupeana mkono na mwanamme ajnabiy pamoja juu ya kuwa mwanamke amevaa glavu katika mikono yake?

 

 

Jibu:

 

Wanawake kupeana mikono na wasiokuwa mahaarim ni haraam iwe kuwa amevaa kizuizi kama vile glavu au asiwe amevaa kizuizi. Hata hivyo bila ya kizuizi ni hatari tena hatari mno, hivyo si halaal kwa mwanamke kumpa mkono mwanamme ambaye si mahrim wake. Ama walio maharim wao, basi hao sio neno kuwapa mikono kwa sharti kuaminisha fitna vile vile kuwa hawezi kuangukia kwenye fitna, ama itakapoonekana kuwa huenda ikapelekea katika fitna katika kupeana mkono na Maharim basi itabidi kuacha kufanya hivyo.

 

[Fataawaa Nuwr ‘Ala-Darb (246)]

 

 

 

Share