21-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah (عزّ وجلّ) Ameapia Kwa Uhai Wake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

21-Allaah (عزّ وجلّ) Ameapia Kwa Uhai Wake

www.alhidaaya.com

 

Allaah (‘Azza wa Jalla)      Hajapatapo kuapia kwa uhai wa mtu yeyote katika waja Wake isipokuwa kwa uhai wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hii ni kutokana na Sharaf na taadhima kubwa Aliyomjaalia Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ﴿٧٢﴾

Naapa kwa uhai wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم!) Hakika wao walikuwa katika ulevi wao wanatangatanga kwa upofu. [Al-Hijr: 72]

 

 

Imehadithiwa kutoka kwa ‘Amr bin Maalik An-Nakriy kutoka kwa Abuu Al-Jawzaa kwamba Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema:  “Allaah Hajapatapo kuumba wala kuanzisha wala kuunda roho ambayo ni kipenzi Kwake kama roho ya Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Wala sijapatapo kusikia Allaah Ameapia uhai wa yeyote ghairi yake.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]   

 

 

Share