Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Aashuraa: Aanze Swiyaam Za ‘Aashuraa Au Alipe Swiyaam Za Ramadhwaan?

 

 

Aanze Swiyaam Za ‘Aashuraa Au Alipe Swiyaam Za Ramadhwaan?

 

Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

 

Ikikusanyika kufanya ya waajib (kulipa deni la Ramadhwaan) na yaliyo mustahabb (yanayopendezeka au yanayosisitizwa) na ikawafikiana na wakati wa mustahabb je inampasa mtu afanye yaliyo mustahabb na alipe yaliyo waajib baadae au  afanye waajib au laa? Kwa mfano: Siku iliyowafikiana na  ‘Aashuraa kufunga na kulipa deni la Swiyaam za Ramadhwaan?

 

JIBU:

 

 

Kuhusu kufunga Swiyaam za faradhi na Swiyaam za Sunnah, kipaumbele ni kuanza kufunga Swiyaam za faradhi kisha baada yake za Sunnah kwani Swiyaam za faradhi ni deni lenye kuwajibika kwake. Ama Swiyaam za  Sunnah ni ya kujitolea na kama hajafunga si neno kwake, na kwa haya tunamwambia ambaye ana deni la Swiyaam za Ramadhan “Funga lililo katika deni lake kabla ya kufunga Sunnah.”

 

 

Ama Swawm yake Sunnah  ni sahihi ikiwa muda upo wa kutosha wa kulipa. Kwa sababu muda wa kulipa unakwenda hadi kukaribia kabla ya Ramadhwaan ijayo inapofika. Ikiwa kuna muda wa kutosha upo basi Swawm ya Sunnah  inaruhusiwa. Kwa mfano wa Swalaah ya faradhi kama muda wa kutosha wa kuswali Sunnah basi anaswali. Kwa mfano mtu anafunga ‘Arafah au siku ya ‘Aashuraa na ana deni la Swawm ya Ramadhwaan basi Swawm yake ni sahihi. Lakini akinuwia kufunga siku hii kwa lengo la kulipa Ramadhwaan, mtu huyu ana ujira mara mbili:

 

  1. Ujira wa siku ya ‘Arafah
  2. Ujira wa siku ya ‘Aashuraa pamoja na ujira wa kulipa.

 

Hii ni kwa mujibu wa Swawm ya Sunnah ambayo haihusiani na Ramadhwwan. Ama Swiyaam za  Sitta Shawwaal, hii imeunganishwa na Ramadhwaan na haiwezi kutekelezwa ila baada ya kulipa deni la Ramadhwwan. Lau akifunga kabla ya kulipa hatopata malipo yake, kwa kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  “Atakayefunga Ramadhwaan  kisha akafuatilia na Sitta ya Shawwaal ni kama kwamba amefunga mwaka mzima.” 

 

Kinafahamika kuwa yule mwenye deni la kulipa basi hachukuliwi kuwa amefunga Ramadhwaan hadi akamilishe madeni yake.  Na  kuhusu masuala haya, baadhi ya watu hudhani kuwa kama mtu anaogopea kuondoka kwa Shawwaal kabla ya kufunga Sitta, basi hufunga na hata kama deni bado lipo na hili ni kosa kwani Sunnah hii haifungwi isipokuwa ni baada ya mtu kukamilisha Swiyaam za  Ramadhwaan.

 

[Fataawaa Ash-Shaykh bin ‘Uthaymiyn Mjeledi 20]

 

 

Share