Skip to main content

Hukumu ya Udhwhiya kwa Maiti

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) amesema:

a-Udhwhiya ni kwa walio hai. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alikuwa na ndugu waliokufa kabla lakini hakuwachinjia.

b-Atakapousia mtu kabla ya kufa kwake achinjiwe basi usia wake utafuatwa  na atachinjiwa.

c-Achinje mtu kwa ajili yake na watu wa nyumbani kwake na anuie hilo walio hai na waliokufa.

d-Maiti kupwekeka na Udhwhiya si katika Sunnah.

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/11]