39-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ni Upi Muda Wa Mwisho Wa Swalaah Ya ‘Ishaa Na Vipi Kuujua

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

39-Ni Upi Muda Wa Mwisho Wa Swalaah Ya ‘Ishaa Na Vipi Kuujua

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Ni upi muda wa mwisho wa Swalaah ya ‘Ishaa, na vipi kuujua muda wenyewe?

 

 

JIBU:

 

Mwisho wa wakati wa ‘Ishaa ni katikati ya usiku na wakati wenyewe unaweza kuujua kwa kuugawa kati ya muda wa Magharibi na muda wa Swalaah ya Alfajiri. Nusu ya kwanza inaisha wakati wa Swalaah ya ‘Ishaa. Na nusu ya pili inayobaki haikadiriwi kwa wakati bali kwa kitenganisho baina ya ‘Ishaa na Alfajiri.

 

 

Share