058-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah Aayah 058: وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ

 

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

At-Tawbah: Aayah 58

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ فَإِنْ أُعْطُوا مِنْهَا رَضُوا وَإِن لَّمْ يُعْطَوْا مِنْهَا إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ﴿٥٨﴾

Na miongoni mwao wako wanaokufedhehesha kwa kushutumu katika (ugawaji wa) Swadaqah. Wakipewa humo wanaridhika, na wasipopewa humo tahamaki wao wanaghadhibika.

 

وَلَوْ أَنَّهُمْ رَضُوا مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ سَيُؤْتِينَا اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَرَسُولُهُ إِنَّا إِلَى اللَّـهِ رَاغِبُونَ﴿٥٩﴾

Na lau wangeliridhiya yale Aliyowapa Allaah na Rasuli Wake, na wakasema: Anatutosheleza Allaah, karibuni Allaah Atatupa katika fadhila Zake na Rasuli Wake (pia); hakika sisi kwa Allaah tuna raghba.   [At-Tawbah: 58-59]

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 
 حدثنا عبد الله بن محمد حدثنا هشام أخبرنا معمر بن الزهري عن أبي سلمة عن أبي سعيد قال: بينما النبي صلى الله عليه وعلى آله وسلم يقسم جاء عبد الله بن ذي الخويصرة التميمي فقال: اعدل يا رسول الله، فقال: "ويلك من يعدل إذا لم أعدل". قال عمر بن الخطاب:      دعني أضرب عنقه، قال: "دعه فإن له أصحابا يحقر أحدكم  صلاته مع صلاته وصيامه مع صيامه يمرقون من الدين كما يمرق السهم من الرمية ينظر في قذذه فلا يوجد فيه شيء ثم ينظر في نصله فلا يوجد فيه شيء ثم ينظر في رصافه فلا يوجد فيه شيء ثم ينظر في نضيه فلا يوجد فيه شيء قد سبق الفرث والدم، آيتهم رجل إحدى يديه أو قال ثدييه مثل ثدي المرأة أو قال مثل البضعة تدردر يخرجون على حين فرقة من الناس". قال أبو سعيد أشهد سمعت من رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم وأشهد أن عليا قتلهم وأنا معه جيء بالرجل على النعت الذي نعته رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم قال: فنزلت فيهم  وَمِنْهُمْ مَنْ يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ

 

Ametuhadithia ‘Abdullaah bin Muhammad, ametuhadithia Hishaam, ametueleza Ma’amar toka kwa Az-Zahriy toka kwa Abuu Salamah toka kwa Abuu Sa’iyd amesema: Wakati Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  anagawa, alikuja ‘Abdullaah bin Dhiy Al-Khuwayswirah At-Tamiymiy akasema: Fanya uadilifu ee Rasuli wa Allaah. Akasema: “Ole wako! Nani atafanya uadilifu kama mimi sikufanya uadilifu?!” ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Niruhusu nimkate shingo yake. Akamwambia: “Mwache, yeye ana wenzake, mmoja wenu anaiona Swalaah yake si chochote kulinganisha na Swalaah  yake, na Swiyaam yake (si chochote) na Swiyaam yake (kwa jinsi wanavyozipamba ‘ibaadah hizo), wanachomoka toka kwenye Dini kama unavyotoka mshale upande wa pili wa mnyama aliyepigwa nao. Ukiangaliwa unyoya wake hakionekani kitu, kisha kikiangaliwa chembe chake hakionekani kitu, kisha ukiangaliwa utepe wake hakionekani kitu, kisha ukiangaliwa ujiti wake hakionekani kitu na hali mshale umepita kwenye kinyesi na damu (bila kuonekana athari yake). Alama yao ni mtu ambaye mkono wake mmoja (au kasema maziwa yake mawili) ni mithili ya titi la mwanamke, (au kasema mfano wa kipande cha nyama kinachocheza cheza), wanatoka katika wakati utakapotokea mfarakano wa watu (Waislamu). Abuu Sa’iyd amesema: Ninashuhudia nimesikia toka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    na ninashuhudia kuwa ‘Aliy aliwaua mimi nikiwa pamoja naye, aliletewa mtu mwenye sifa zile zile alizozielezea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).    Akasema ikateremka kuhusu wao:

 وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ

 

[Al-Bukhaariy]

Share