46-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Ametanguliza Kumtaja Yeye Katika Qur-aan Kabla Ya Manabii Wengineo

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

46-Allaah Ametanguliza Kumtaja Yeye Katika Qur-aan Kabla Ya Manabii Wengineo

 

www.alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa fadhila zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) amemtanguliza Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kumtaja kabla ya Manabii wengineo au kumlinganisha na Manabii wengine katika Aayaat za Qur-aan kadhaa, miongoni mwazo ni kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٧﴾

Na pale Tulipochukua kutoka kwa Manabii fungamano lao na kutoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na kutoka kwa Nuwh, na Ibraahiym, na Muwsaa, na ‘Iysaa mwana wa Maryam; na Tukachukua kutoka kwao fungamano gumu. [Al-Ahzaab: 7]

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾

Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na dhuriya, na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, Na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr. [An-Nisaa: 163]

 

Share