47-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kutimiza Akhlaaq (Tabia) Njema

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

47-Ametumwa Kutimiza Akhlaaq (Tabia) Njema

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ametumwa kutimiza Akhlaaq (tabia):

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ الله عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ‏:‏ ((إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ صَالِحَ الأَخْلاقِ‏))

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    amesema: ((Hakika nimetumwa ili nikamilishe khulqa (tabia) njema)) [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy Swahiyh Al-Jaami’ (2349), Swahiyh Adab Al-Mufrad (207)]

 

Ni fadhila adhimu kabisa kujaaliwa yeye mtu mmoja, Nabiy wa mwisho ili akhlaaq hizo ziwe kigezo wa walimwengu wote waliobakia mpaka Siku ya Mwisho ili kwa atakayemwamini na kumfuata iwe ni sababu ya kufaulu kwake duniani na Aakhirah.

 

Hivyo basi, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akadhihirisha Akhlaaq zake ambazo ni kigezo na sifa za kujinasabisha nazo Muumin wa kweli na akataja katika Hadiyth zake kadhaa kuwa Akhlaaq njema ni sababu kuu ya kumfikisha mtu katika Jannaatul-Firdaws karibu naye, na haya ndio mafanikio adhimu kabisa ya kupaswa kuyaazimia kwa nguvu. Mfano wa Hadiyth aliyothibitisha kabisa kuwa Akhlaaq njema zitakuwa ni nzito kabisa katika Miyzaan ya mja Siku ya Qiyaamah:

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( مَا مِنْ شَىْءٍ أَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ حُسْنِ الْخُلُقِ ‏))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ad-Dardaai kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitakachokuwa kizito katika Miyzaan kama Husnul-Khuluq [tabia njema])) [Sunan Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (2/535), Swahiyh Al-Jaami’ (5721), Swahiyh Adab Al-Mufrad (204)]

 

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate Hadiyth tele zenye kutaja Akhlaaq (tabia) zake (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

 

Share