51-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amefunuliwa Wahyi Mbingu Ya Saba; Suwrah Na Aayah Mbili Ambazo Hajapewa Nabii Yoyote Kabla Yake

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

51-Amefunuliwa Wahyi Mbingu Ya Saba; Suwrah Na Aayah Mbili

Ambazo Hajapewa Nabii Yoyote Kabla Yake  

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amepewa katika Qur-aan Suwrah Al-Faatihah na Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah, ambazo hajapatapo kupewa mfano wa kama Aayah hizo Nabiy mwenginewe kabla yake.  Juu ya hivyo, Aayah hizo amefunuliwa nazo Wahyi akiwa mbingu ya Saba katika safari ya Israa wal-Mi’raaj:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ فَرَفَعَ رَأْسَهُ فَقَالَ: ((هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ فَقَالَ: هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَسَلَّمَ وَقَالَ أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ، فَاتِحَةُ الْكِتَابِ وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلاَّ أُعْطِيتَهُ)) ‏.‏

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)   amehadithia kwamba: Jibriyl   (عليه السلام)  alipokuwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl   (عليه السلام) akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kufunguliwa isipokuwa leo.” Malaika akateremka humo akasema: “Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo.” Akasalimia kisha   akasema: “Pokea bishara ya nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako; Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah.  Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake ziliomo.” [Muslim]

 

 

Imaam Muslim amenukuu katika Swahiyh yake kuwa Aayah hizi mbili alipewa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika kikomo mbingu ya saba katika Safari ya Al-Israa Wal-Mi’raaj pamoja na kupewa Swalaah tano na msamaha kwa mtu asiyemshirikisha Allaah na yeyote au chochote.

 

 

 

Share