Puri

Vipimo
Unga 3 Vikombe
Mafuta ya zaituni au ya kawaida ¼ kikombe
Chumvi kiasi
Maji ya dafu dafu ½ kikombe takriban
Mafuta ya kukaangia katika karai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya vitu vyote katika bakuli, kisha ukande unga uwe
2. Fanya madonge madogo madogo, kisha yafunike kwa kwa mfuko wa plastiki au kitamba yasipate upepo kwa muda wa dakika 15-20
3. Pasha moto mafuta huku unasukuma madonge yawe kiasi tu.
4. Kaanga madonge ukitia moja moja au mawili mawili inategemea na ukubwa wa karai. Kaanga hadi yafure na kubadilika rangi.
5. Epua na yatie katika chujio yatoke mafuta yakiwa tayari kuliwa.
Kidokezo : Puri nzuri kuliwa na kuku wa kuchoma na sosi zake
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


