Khalyat An-Nahl (Mzinga Wa Nyuki)

Vipimo
Maziwa ya maji Vikombe 1
Maji Kikombe ½
Yai 1
Sukari Vijiko 2 ½ vya supu
Mafuta Kikombe ½
Hamira Kijiko ½ cha chai
Chumvi robo kijiko cha chai
Cheese ya Cream Kiasi utakavyotumia kujaza
SHIRA
Sukari Vikombe 2
Maji Kikombe 1 ½
Zaafarani nusu kijiko cha chai (iroweke)
Ipikie shira lakini isiwe nzito.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya vitu vyote hivyo isipokuwa cream cheese.
2. Kanda kidogo tu kulainisha unga uwe mlaini
3. Pakaza siagi katika sinia ya round utakayopikia
4. Fanya viduara vidogo vidogo na tia ndani yake cheese ya cream kwa kutumia kijiko cha chai, na vifunge viduwara vizuri na kuvipanga katika sinia bila ya kuwacha nafasi.
5. Iwache ifure
6. Ipikie katika oven moto wa chini kwanza katika 350 Deg, kwa muda wa baina dakika 20 na 25 . Kisha washa moto wa juu kidogo tu uwive kwa juu.
7. Toa katika oven na mwagia shira
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


