09-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْواحِدُ - الأَحَدُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

 الْواحِدُ - الأَحَدُ

 

 

 

الْواحِدُ

Al-Waahid

Mmoja Pekee Asiye Na Mfano

 

 

 

الأَحَدُ

Al-Ahad

Mpweke Asiye Na Mshirika

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى), Yeye Ndiye Mmoja wa Pekee katika vipengele vyote vya ukamilifu kiasi kwamba hakuna chochote chenye kushirikiana Naye katika hayo. Ni jambo la lazima kwa waja kumpwekesha Yeye Peke Yake katika iymaan, maneno na matendo kwa kutambua ukamilifu Wake usio na mipaka, Tawhiyd Yake na kumpwekesha katika namna zote za ‘ibaadah.

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu Nabiy Yuwsuf aliposema:

 

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ﴿٣٩﴾

Enyi masahibu wangu wawili wa jela. Je, miola wengi wanaofarakana ni bora au Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika? [Yuwsuf (12): 39]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

Sema: Yeye ni Allaah Mmoja Pekee[Al-Ikhlaas (112): 1]

 

 

Share