44-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْحَيُّ - الْقَيُّومُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْحَيُّ - الْقَيُّومُ

 

الْحَيُّ

Al-Hayyu

Aliye Hai Daima

 

 

الْقَيُّومُ

Al-Qayyuwm

Msimamizi Kila Jambo Milele

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Aliye na nguvu kamilifu, zipo za Kwake Mwenyewe na hamtegemei mwingine yoyote. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mwenye kuruzuku wakazi wa mbinguni na ardhini, ni Pekee Anayedhibiti mambo yao na rizki zao. Jina Al-Hayyu linajumuisha Sifa zote za Nafsi Yake na Jina Al-Qayyuwm linajumuisha Sifa zote Matendo Yake.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa; Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah (2): 255]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

الم ﴿١﴾

Alif Laam Miym.

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴿٢﴾

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu.

 

 نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾

Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na AkateremshaTawraat na Injiyl.

 

 

مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾

Kabla (ya kuteremshwa Qur-aan), iwe ni mwongozo kwa watu na Akateremsha pambanuo (la haki na batili). Hakika wale waliokufuru Aayaat za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kuangamiza.

[Aali ‘Imraan (3): 1-4]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْمًا ﴿١١١﴾

Nyuso zitanyenyekea kwa Aliye Hai daima, Msimamizi wa kila kitu. Na kwa yakini ameharibikiwa abebaye dhulma. [Twaahaa (20): 111]

 

 

 

 

Share