61-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hukmu Zake Za Shariy’ah Ni Sawa Na Hukmu Za Qur-aan

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

61-Hukmu Zake Za Shariy’ah Ni Sawa Na Hukmu Za Qur-aan

 

Alhidaaya.com

 

 

Hukmu za Shariy’ah anazotoa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni sawa na hukmu za Qur-aan kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Amemteremshia Qur-aan kisha Akamtaka yeye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awabainishie watu ili Qur-aan na hukmu zake zifahamike kwa watu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾

 (Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari. [An-Nahl: 44]

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akamjaalia kumpa  mfano wa Qur-aan, kisha  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akatahadharisha watu wasije kudai kuwa Qur-aan inawatosheleza kama wanavyodai kundi potofu linalojulikana kwa Qur-aaniyyuwn wanaoamini Qur-aan lakini wanapinga Ahaadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

 

((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ، أَلَا يُوشِكُ رَجُلٌ يَنْثَنِي شَبْعَانًا عَلَى أَرِيكَتِهِ يَقُولُ: "عَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَلَال فَأَحِلُّوهُ وَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِمِنْ حَرَامٍ فَحَرِّمُوهُ... ((رواه أبو داود والترمذي والحاكم وصححه وأحمد بسند صحيح

“Tanabahi! Hakika nimepewa Qur-aan na inayofanana nayo (Sunnah) Tanabahi! Utafika wakati mtu aliyeshiba mno ataegemea kwenye kochi na kusema: “Shikamaneni na Qur-aan, mtakayokuta humo ya halaal halalisheni, na mtakayokuta ya haraam haramisheni.” [Imepokewa na Abu Daawuwd, na At-Tirmidhiy, na Al-Haakim na ameisahihisha Ahmad kwa isnaad Swahiyh].

 

Na akasema pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth:

 

عَنْ أَبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((كُلُّ أُمَّتِي يَدخُلُونَ الجَنَّةَ إلا مَنْ أبَى)). قيلَ: وَمَنْ يَأبَى يَا رَسُول الله؟ قَالَ: ((مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أبَى)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Ummah wangu wote wataingia Jannah isipokuwa atakayekataa.” Akaulizwa: Ni yupi atakayekataa Ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Atakayenitii mimi ataingia Jannah, na atakayeniasi basi amekataa.” [Al-Bukhaariy]

 

Na kumtii kwake amri na hukmu zake ni sawa na kumtii Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyoamrisha Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٣٢﴾

Na mtiini Allaah na Rasuli mpate kurehemewa. [Aal-‘Imraan: 132]

 

Na katika Hadiyth:

 

 

عَنْ أبي هُرَيْرة رضى الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ مَنْ أَطَاعَنِي فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللَّهَ، وَمَنْ أَطَاعَ أَمِيرِي فَقَدْ أَطَاعَنِي، وَمَنْ عَصَى أَمِيرِي فَقَدْ عَصَانِي ‏"‏‏.‏

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amehadithia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayenitii basi atakuwa amemtii Allaah, na atakayeniasi atakuwa amemuasi Allaah, na atakayemtii Amiri wangu (kiongozi niliyemteua), atakuwa amenitii mimi na atakayemuasi atakuwa ameniasi mimi.” [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]

  

Na Aayah nyenginezo kadhaa zinazothibitisha kuwa inapasa kumtii Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kila alichokuja nacho na kuwaamrisha Waumini, na kwamba ana haki ya kutoa hukmu ikawatosheleza Waislamu. Miongoni mwa Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) ni zifuatazo:

 

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا﴿٦٥﴾

“Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha kikamilifu.” [An-Nisaa: 65]

 

 

Na pia,

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa: 59] 

 

 

Na pia,

 وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ

Na lolote analokupeni Rasuli ((صلى الله عليه وآله وسلم  basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allaah. [Al-Hashr: 7]

 

Na pia,

 

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾

Na haiwi kwa Muumini mwanamume na wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana hiari katika jambo lao.  Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka upotofu bayana. [Al-Ahzaab: 36]

 

 

Na kwa kuwa ayasemayo ni Wahyi kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

مَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Na wala hatamki kwa hawaa. Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

 

 

 

Share