Imaam Al-Albaaniy: Kusema BismiLLaah Wakati Wa Kutia Wudhuu Ni Waajib

Kusema BismiLLaah Wakati Wa Kutia Wudhuu Ni Waajib

 

Imaam Al-Albaniy (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayh wa aalihi wa sallam) amesema:

لَا وُضُوءَ لِمَنْ لَمْ يَذْكُرِ اِسْمَ اَللَّهِ عَلَيْهِ

‘’Hakuna wudhuu kwa asiyetaja Jina la Allaah wakati wa kutawadha’’

 

Amesema Imaam Al-Albaniy (Rahimahu Allaah):

 

“Wajibu wa kusema ni kinachotolewa dalili juu yake na hakuna dalili inapoelekea kutoka juu ya dhahiri yake kuelekea kwenye kauli ya kuwa jambo hili ni mustahabbu, kwani imethibiti uwajibu wake na hii ni kwa mujibu wa madhehebu ya Adhwahiriyya, Is-haaq na moja katika Riwaayah mbili kutoka kwa Ahmad ambayo ameichagua Swiddiyq  Khan, Ash-Shawkaniy nayo ni kweli In Shaa Allaah.” [Tamaam Al-Minnah (89)]

 

 

Share