13-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Ubora Wa ‘Aalim- Allaah Na Viumbe Wote Wanamuombea Mwenye Kufundisha Khayr

 

Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

 

Hadiyth Ya 13

 

Ubora Wa ‘Aalim -  Allaah Na Viumbe Wote Wanamuombea (Maghfirah Na Kila Khayr)

Mwenye Kufundisha Watu Mambo Ya Khayr (Ya Dini Ya Kiislaam)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ (رضي الله عنه) أنَّ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((فضْلُ الْعَالِمِ عَلَى الْعَابِدِ كَفَضْلِي عَلَى أَدْنَاكُم))  ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((إِنَّ اللَّهَ وَمَلاَئِكَتَهُ وَأَهْلَ السَّمَوَاتِ وَالأَرَض حَتَّى النَّمْلَةَ فِي جُحْرِهَا وَحَتَّى الْحُوتَ لَيُصَلُّونَ عَلَى مُعَلِّمِي النَّاسِ الْخَيْرَ)) رواه الترمذي  وقَالَ حَدِيثٌ حَسَنٌ.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Umaamah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: “Ubora wa ‘Aalim (Mwanazuoni) juu ya mfanya ‘Ibaadah, ni kama ubora wangu juu ya mwenye daraja ya chini miongoni mwenu.” Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika Allaah na Malaika Wake, na walio mbinguni, hata wadudu chungu waliomo katika mashimo yao, na hata samaki, wanawaombea (maghfirah na khayr) wanaowafundisha watu kheri.” [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan]

 

 

 

 

Share