18-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Allaah Huichukua ‘Ilmu Kwa Kufariki ‘Ulamaa Kisha Viongozi Wajinga Watatoa Fatwa Bila ‘Ilmu

Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

 

Hadiyth Ya 18

Allaah Huichukua ‘Ilmu Kwa Kufariki ‘Ulamaa

Kisha Viongozi Wajinga Watatoa Fatwa Bila ‘Ilmu

 

Alhidaaya.com

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ "‏ إِنَّ اللَّهَ لاَ يَقْبِضُ الْعِلْمَ انْتِزَاعًا، يَنْتَزِعُهُ مِنَ الْعِبَادِ، وَلَكِنْ يَقْبِضُ الْعِلْمَ بِقَبْضِ الْعُلَمَاءِ، حَتَّى إِذَا لَمْ يُبْقِ عَالِمًا، اتَّخَذَ النَّاسُ رُءُوسًا جُهَّالاً فَسُئِلُوا، فَأَفْتَوْا بِغَيْرِ عِلْمٍ، فَضَلُّوا وَأَضَلُّوا ‏"‏‏.

Abdallaaah bin Amr bin Al-Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia:    Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Allaah Haiondoshi ‘Ilmu kwa kuichukua kutoka kwa (mioyo ya) watu,  lakini Huichukua kwa kufariki ‘Ulamaa mpaka watakapokwisha (‘Ulamaa) wote, watu watachukua kama wao viongozi wajinga  ambao wataulizwa na watatoa Fatwa bila ‘Ilmu. Kwa hiyo watapotoka na watapotosha (Ummah). [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share